Home BUSINESS NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA MIUNDOMBINU YA GESI SONGOSONGO

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA MIUNDOMBINU YA GESI SONGOSONGO




Na: Zuena Msuya, Lindi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ametembelea na kukagua miundombinu ya Mradi wa kuzalisha na kuchakata Gesi asilia wa Songosongo uliopo Mkoani Lindi.

Mahimbali amesema kuwa lengo la ziara hiyo iliyofanyika Machi 31, 2022 ni kutaka kuona shughuli za uzalishaji, uchakataji na usafirishaji wa Gesi asilia kutoka katika visima vya Gesi vilivyopo katika eneo la bahari nan chi kavu katika eneo hilo.

Katika ziara hiyo ametembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Songosongo, eneo ililofungwa mtambo mpya wa kuongeza mgandamizo wa Gesi asilia, pamoja na Kisima namba kumi (10) kinachofanyiwa ukarabati.

Aidha alitembelea kisima namba nne (4),(12), 11 pamoja na  sehemu ambayo gesi inayozalishwa kutoka visimani inasafirishwa kuingia katika bomba la kusafirisha Gesi asilia kwenda Somangafungu hadi Kinyerezi,  Dar es salaam kwa ajili ya kuzalisha Umeme na matumizi mengine.

Eneo lingine alilotembelea ni eneo la kupokelea gesi kutoka katika visima vya gesi inapochakatwa, sehemu ya kuongeza mgandamizo wa gesi asilia (compression) pamoja na chumba maalum cha kuendeshea mitambo ya gesi asilia (Control room). 

Katika ziara hiyo ameambatana na Viongozi waandamizi kutoka Wizarani na Kampuni Tanzu ya kusimamia Gesi(GASCO) ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC).

Picha mbalimbali zikimuonyesha Naibu Katibu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya mradi wa gesi asilia ya Songosongo mkoani Lindi.
Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO IJUMAA APRILI 1-2022
Next articleLIVE: MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM, DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here