Home Uncategorized SAKATA LA MACHINJIO VINGUNGUTI KUSUA SUA MADIWANI ILALA WALIAMSHA

SAKATA LA MACHINJIO VINGUNGUTI KUSUA SUA MADIWANI ILALA WALIAMSHA

  NA: HERI SHAABAN(ILALA)

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo wametaka waelezwe lini mradi wa  machinjio ya kisasa VINGUNGUTI yanafunguliwa rasmi .

MADIWANI hao wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walitoa hoja hiyo Katika kikao cha Baraza la Madiwani katika maswali ya papo kwa papo ambapo hoja hiyo iliungwa mkono na madiwani wote.

Akizungumza katika Baraza hilo Mbunge wa Viti Maalum Janeth Masaburi alisema ujenzi wa mradi wa machinjio ya VINGUNGUTI Kila siku unasua hatima yake bado kufamika tunaomba tuelezwe ukweli ikishindikana tuombe Serikali Kuu itusaidie.

“Tunaomba tuelezwe ukweli kusuasua kuanza kazi ya kufunguliwa Machinjio ya kisasa VINGUNGUTI tujue unamalizika lini  mradi huu mkubwa wa  Serikali mda wake ulitakiwa ukabidhiwe umepita mpaka leo kimya “alisema Masaburi.

Mbunge Masaburi aliomba miradi huo ukabidhiwe pamoja na miradi mingine yote imalizike kwa wakati kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mwanamke Samia Suluhu Hassan katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Katika Baraza hilo Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam waliunga mkono hoja hiyo  kufatilia Maendeleo ya miradi ya Machinjio wakitaka Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Meya kuchukua hatua kufatilia kujua ujenzi huo umekwama  kwanini mpaka sasa ujafunguliwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu alisema Kikao Cha Kamati ya fedha na Utawala  na kutoa maelekezo ndani ya miezi mitatu machinjio hayo yawe yamefunguliwa.

Tabu Shaibu alisema miezi mitatu hiyo inaanza  mwezi Machi mwaka huu hadi Mei mwaka huu yatakuwa yamemalizika.

Mwisho.

[3/3, 6:48 PM] Kheri Shaaban: Mbunge wa Viti Maalum Janeth Masaburi akizumza Katika kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Machi 02./2022 katika Kikao hicho Mbunge Masaburi aliuliza kuhusu kusua sua kufunguliwa Machinjio ya kisasa VINGUNGUTI Wilayani Ilala (PICHA NA HERI SHAABAN)

Previous articlePOLISI TANZANIA YAPANIA KUFUFUKIA KWA AZAM.
Next articleHALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI MKOA WA SINGIDA YAZIDI KUNG’ARA KITAALUMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here