Na. Costantine James, Geita.
Mtoto wa maiaka 7 John Frank Mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi nguzo mbili Mkoani Geita amefariki dunia wakati akipelekwa hosibitalini kupatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara kuelekea shuleni.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Geita kamishina msaidizi Henry Mwaibambe emedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari iliyosababisha ajali hiyo.
Mwaibambe amesema mpaka sasa wanamshikilia dereva wa gali lililo sababisha ajali lenye usajili namba T 177 AHH, aina ya Isuzu Tipa dereva huyo ametambulika kwa jina la Renatus Christopher mwenye umri wa miaka 31 wanamshikilia kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda Mwaibambe amesema eneo hilo linawatu wengi kutokana na kuwepo shule mbili katika eneo hilo, Shule ya Msingi Nguzo mbili, Shule ya msingi Mwatule amesema kufuatia ajali hiyo jeshi la polisi wamechukua hatua ya kuweka asikali wa usalama barabarani ili kuwavusha watoto katika eneo hilo.
“Imetokea ajali leo majira ya saa tano asubuhi eneo la mwatulole ambapo mtoto wa darasa la kwanza aitwaje John Frank mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Nguzo Mbili amefaliki dunia wakati akipelekwa hosipitali kupatiwa matibabu hospitalini” Amesema Kamanda Mwaibambe.
Baadhi ya wananchi wa Mwatulole ambao ni mashuhuda wa ajali hiyo wamesema eneo hilo limekuwa hatalishi kutokana na kuwepo kwa wanafunzi wengi.
Wananchi pamoja na wazazi wameiomba serikali kuweka alama za barabarani katika eneo hilo ili kupunguza ajali kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Nguzo mbili na mwatulole kwani madereva wa malori wamekuwa wakipita kwa kasi katika eneo hilo.