Home Uncategorized MASHABIKI 35,000 WARUHUSIWA MECHI YA SIMBA SC NA GENDARMARIE KWA MKAPA

MASHABIKI 35,000 WARUHUSIWA MECHI YA SIMBA SC NA GENDARMARIE KWA MKAPA


Picha Na: Emmanuel Mbatilo

NA: EMMANUEL MBATILO, Fullshangwe Blog, DAR

KLABU ya Simba imeruhusiwa kuingiza mashabiki takribani 35,000 kwenye mchezo wake wa nyumbani wakiwakaribisha timu  ya US Gendarmerie mchezo ambao utapigwa tarehe 03/04/2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Simba Sc, Bw.Ahmed Ally amesema tiketi tayari zinauzwa mitandaoni na kwa mashabiki wetu waliopo mikoani hakuna haja ya kununua tiketi hadi wakifika Dar es Salaam.

“Tumeruhusiwa mashabiki 35,000. Awali tuliomba kuongeza idadi ya mashabiki kupitia kwa TFF lakini kwa sababu ya mambo ya Covid wameruhusu idadi ya mashabiki 35,000. Mashabiki ambao wanataka kuja kuona mchezo wanunue tiketi mapema.” Amesema Bw.Ahmed Ally

Amesema wataingia kwenye mchezo wa jumapili wakiwa na lengo moja ushindi na wanaimani watashinda na kutinga hatua ya robo fainali.

Aidha amesema siku ya jumatano watakuwa standi ya Magufuli watakuwa pale kwa pamoja na mgeni wetu rasmi atakuwa ni Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu.

“Tukio letu la jumatano kwenye stendi ya Magufuli itakuwa saa 4 hadi 5 asubuhi. Tunakutana pale kufurahi, kushangilia Simba yetu”. Amesema Ahmed Ally.

Credit – Fullshangwe Blog

Previous articleCHUO KIKUU MZUMBE CHATOA TAARIFA YA VIFO VYA WATUMISHI WAKE
Next articleWAKALA WA MBEGU NCHINI ASA WATAKIWAA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBEGU BORA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here