Na: Lucas Raphael,Tabora
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya amemkaa hakimu katika Shauri la Madai ya fidia ya shilingi milioni 140 ambalo limepingwa kalenda hadi Marchi 31/2022 litakapoanza kusikilizwa baada ya kupangiwa hakimu mwengine .
Komanya alifika uamzi huo jana muda mfupi baada ya Shauri hilo la Madai Namba 04/2021 kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora Nzige Sigwa kwa ajili ya kuanza Kusikilizwa.
Katika maelezo yake Komanya alisema kuwa hana Imani na Hakimu Nzige kutokana na kile alichodai kwamba hakimu huyo aliwahi kutupa mapingamizi yake aliyowasilisha Mahakamani hapo.
Hakimu Sigwa mara baada ya kupokea hoja hiyo ya Komanya ambaye ni Mdaiwa katika shauri hili pamoja na kuyakubali lakini alionyesha kusikitishwa na kitendo hicho ambacho alikiita cha kuipotezea muda mahakama.
Kufuatia maombi hayo Mahakama ya Wilaya ya Tabora Imeahirisha hadi Marchi 31 /2022 shauri hilo la Madai iliapangiwe Hakimu mwingine kwa ajili ya kulisikiliza baada ya kushindikana katika hatua ya Usuluhishi.
Mdai katika Shauri hili Alex Ntonge alifungua kesi mahakamani anataka alipwe kiasi cha shilingi milioni 140 kama fidia kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa na Komanya wakati akiwa ni Mkuu wa Wilaya.
Ntonge kupitia kwa wakili wake Kelvin Kayaga anadai alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa na Komanya Januari 05/2021.
Anadai kuwa siku hiyo Komanya ambaye wakati huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askali wa jeshi la Polisi walifika nyumbani kwake na Kumdhalilisha.
Aliongeza kuwa siku hiyo akiiwa na askali wenye Silaha baada ya kufika nyumbani hapo walimkamata mdai Ntonge na kisha walimfanyia vitendo vinavyodhalilisha utu wake mbele ya famiria yake na majirani zake.
Ntonge kupitia kwa wakili wake Kelvin Kayaga aliiambia Mahakama kuwa anatarajia kuleta Mashahidi wasiopungua Saba huku Komanya akiwakilishwa na wakili Justine Sikon akidai kuleta mashahidi sita wa utetezi.
Shauri hilo dhidi ya Komanya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora ambaye Uteuzi wake ulikoma juni19 mwaka huu baada ya kuenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan limefunguliwa na Alex Ntonge mkazi wa Mjini hapa.
MWISHO.