Home LOCAL WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA TUZO ZA WANAMICHEZO WALIOFANYA VIZURI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA TUZO ZA WANAMICHEZO WALIOFANYA VIZURI

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 01, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa zinazoandaliwa na Baraza la Michezo Taifa.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Lengo la tuzo hizo ni kuwaenzi na kuwatambua watanzania wanaiowakilisha nchi katika michezo mbalimbali duniani na kuiletea sifa Tanzania kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza Katika hafla hiyo,inayofanyika katika ukumbi wa Superdome Masaki, Jijini Dar es Salaam Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita itaendelea kuwekeza katika sekta ya michezo kwa kuwa inatambua michezo ni afya, ajira, mshikamano, maendeleo lakini pia michezo ni burudani.

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Majaliwa alipokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia tuzo ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia alikabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia michezo nchini.