Home LOCAL RAIS SAMIA AKUTANA NA TUNDU LISSU UBELGIJI

RAIS SAMIA AKUTANA NA TUNDU LISSU UBELGIJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanasiasa ambaye pia ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Antiphas Lissu leo tarehe 16 Februari, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwanasiasa ambaye pia ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Antiphas Li leo tarehe 16 Februari, 2022 katika Jiji la Brussels nchini Ubelgiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Tundu Lissu Jijini Brussels nchini Ubelgiji leo Jumatano Februari 16,2022.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus, amesema Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia kukubali maombi ya kiongozi huyo wa Chadema kukutana naye na kuzungumza jijini Brussels.

Aidha katika mazungumzo hayo Mhe. Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, walizungumza masuala mbalimbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Samia yupo nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi aliyoianza jana.

Previous articleHAKUNA MGOGORO KATI YA WANANCHI NA HIFADHI YA KITULOā€¯ Mhe.Mary Masanja
Next articleSIKU YA PILI UWEKAJI ANWANI YA MAKAZI JIJI LA ARUSHA JAMII YAANZA KUELEWA UMUHIMU WA ZOEZI HILO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here