Home LOCAL MHE. MARY MASANJA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA CCM BUTIAMA

MHE. MARY MASANJA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA CCM BUTIAMA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameshiriki katika maadhimisho ya miaka 45 ya Chama cha Mapinduzi yaliyofanyika katika uwanja wa Mwenge, Wilaya ya Butiama Mkoani Mara leo.

Akizungumza kwa niaba ya Mawaziri na Naibu Mawaziri katika maadhimisho hayo Mhe. Mary Masanja ameahidi kuendelea kutetea maslahi ya wanawake.

“Sisi kama wawakilishi wenu tutahakikisha uwakilishi wetu ni imara katika kutetea maslahi ya wanawake , watoto na vijana na wakati huo huo kuiimarisha jumuiya yetu ya UWT na tuko bega kwa bega kukuunga mkono Mheshimiwa Mwenyekiti.” amesisitiza Mhe. Masanja. 

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuiongoza nchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi na wajumbe wa Umoja wa Wanawake Tanzania kutoka mikoa yote nchini.

Previous articleDC IKUNGI ATOA ONYO KWA WAHALIFU WATAKAOINGIA KATIKA WILAYA HIYO
Next article“ONGEZEKO KUBWA LA SARATANI LINACHANGIWA NA MTINDO WA MAISHA” – WAZIRI UMMY MWALIMU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here