Home LOCAL DC SHIMO AAGIZA VIONGOZI KUSIMAMIA IMARA MIRADI YA...

DC SHIMO AAGIZA VIONGOZI KUSIMAMIA IMARA MIRADI YA MAENDELEO.

 NnNNn

Na: Costantine James, Geita.

Mkuu wa wilaya ya Geita mhe. Wilson Shimo amewataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mtaa, vijiji, kata kusimamia vyema shughuli za ulinzi na usalama wa miundombinu yote  inayoendeshwa katika maeneo yao ili kupunguza wizi wavifaa mbali mbali vya ujenzi vinavyoibiwa hali inayopelekea kuingizi hasara serikali katika utekelezaji wa miuondombinu mbali mbali ya kimaelendeleo katika jamii

Alisema hayo katika mkutano wa wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO’S) uliofanyika katika ukumbi wa alphendo wilayani Geita katika mkoa wa Geita ambapo alisema ulinzi na usalama wa miundombinu ya kimaendeleo inayofanyika katika maeneo mbali mbali katika wialaya hiyo ni vyema viongozi wakashirikiana kuhakikisha ulinzi na usalama wa vifaa mbali mbali vinavyotumika katika miradi hiyo.

Mhe Shimo aliseama serikali imetoa fedha  nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maji ndani ya wilaya ya Geita lakini kunawatu wanafanya uhalibifu wa katika miradi ya maji kutokana na wizi wa vifaa.

“Usimamizi na ulinzi na usalama wa miundombinu yote ya miradi hii ya maji na miradi mingine ni sisi viongozi kwahiyo wito wangu kwa viongozi wa ngazi zote kuanzia mtaa, mwenyekiti wa kitongoji kusimamia vyena shughuli ya ulinzi wa miundombinu yote ya taasisi mbali mbali katika maeneo yao yote”. Alisema Wilson Shimo mkuu wa wilaya ya Geita.

Kwa upande wake Mhandisi Sande Charles meneja wa Ruwasa wilaya ya Geita alikili uwepo wa changamoto ya miundombinu ya maji kuhujumiwa na wananchi kutokana na uhalibifu wanoufanya wa kukata mambomba ya maji unaofanywa  wakati wa shughuli za kilimo pamoja na ufugaji. 

Mhandisi Sande amesema uwepo wa jumuiya za watoa huduma ya maji ngazi jamii imesaidia urahisi wa upatikanaji wa maji kwa kwa jamii kwani jumuiya hizi zinzfanya kazi moja kwa moja na jamii husika hivyo kufanya upatikanaji wa maji nda ya wilaya ya Geita kuongeza kutokana na kuwafikia walengwa moja kwa moja.

“Jukumu la msingi kabisa kwenye hizi jumuiya nikuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama tena endelevu yaani kwa kizazi cha sasahivi na kizazi kijacho”. Alisema mhandisi Sande Charles meneja wa Ruwasa wilaya ya Geita.

Nao baadhi wa wadau wa sekta ya maji waliohudhulia kikao hicho walisema swala la ukataji mambomba katika miundombinu ya maji imekuwa ni changamoto kwao hali inayosababisha baadhi ya maeneo kukosa huduma ya maji kutokana na kukatwa  kwa mambomba yanayosafilisha maji hivyo kusababisha hasara kwa mradi husika.

“Changamoto ni nyingi tunazokutana nazo kwenye mradi wetu watu wanakata mabomba kwa siku tunaweza tukaziba linked hata zaidi ya tatu watua wanakata mabomba bila hata taarifa watu wanao kata mabomba waache hali hiyo inaingiza mradi kwenye hasara pesa ambayo ilikuwa imetengwa kutumika katika matumizi mengine inasababisha tena inunuliwe vifaa ili wazibe” Alisema Rosemary Hamis Fundi bomba.

Previous articleDKT. CHAULA ATOA WITO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
Next articlePATA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO J.PILI FEBRUARI 20-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here