Home LOCAL DKT. CHAULA ATOA WITO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

DKT. CHAULA ATOA WITO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akizungumza na wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Tanga katika kikao chake na Mashirika hayo wakati wa ziara yake Mkoani humo

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Grace Mbwilo akitoa maelezo kuhusu Uratibu wa Mashirika hayo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula.


Sehemu ya washiriki wa kikao cha NGOs Mkoa wa Tanga na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula wakati wa ziara yake Mkoani humo kukagua utekelezaji wa shughuli zinazozimamiwa na Wizara.

Katibu Tawala Wilaya ya Muheza Desderia Haule Nguza akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula alipowasili Wilayani humo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli zinazozimamiwa na Wizara.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Vije Mfaume akiwasilisha taarifa ya shughuli za Maendeleo ya Jamii kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula alipofanya ziara Wilayani humo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli zinazozimamiwa na Wizara.

Na: WMJJWM, Tanga.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula ametoa wito kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kushirikiana na Serikali kuimarisha uchumi na Ustawi wa wananchi.

Dkt. Chaula akizungumza na Mashirika hayo katika Mkoani Tanga amesema Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) ni moja ya chombo muhimu katika nchi hii kinachosimamia NGOs, hivyo kinatakiwa kisimamie vema Mashirika yake.

“KilaShirika lina majukumu lililokusudia, ikiwemo kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, lengo Jamii ibadilike na kurudi kwenye maadili yake” amesema Dkt. Chaula.

Amesisitiza kila slShirika kuangalia sababu ya kujisajili, litekeleze majukumu yake na kufuata kanuni sheria na miongozo iliyopo, ikiwemo kuwasilisha taarifa za kila mwezi.

“Kwa hiyo tunapofanya kazi tunategemea matokeo ambayo kila mwananchi atafurahia uhuru wa nchi hii na Ustawi wa mtu mmoja mmoja utaimarika” Ameongeza Dkt. Chaula.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tanga Saimon Mdende akiwasilisha taarifa ya shughuli zinazofanywa na Idara hiyo amesema mkoa unashirikiana kwa karibu na NGOs kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo kielimisha Jamii madhara ya ukatili wa kijinsia na madawa ya kulevya.

Naye mmoja wa wamiliki wa NGOs ya Gift of Hope Foundation inayoshughulika na kutoa huduma ya ushauri nasaha kwa waathirika wa madawa ya kulevya Said Mbaga, amemueleza Katibu Mkuu malengo ya Taasisi hiyo ni kuhakikisha vijana hawaingii katika mkumbo wa kutumia madawa hayo na waathirika wanapata Huduma na kurudi katika hali zao za kawaida.

Awali, katika Mkutano huo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Muheza, hiyo, Vije Mfaume alisema kwa mwaka 2021/22 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 213 kutoka makusanyo ya ndani kwa ajili kutoa mikopo kwa wajasiriamali Wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu na hadi sasa jumla ya sh. milioni 132 zimetolewa.

MWISHO

Previous articleBRELA YATAKIWA KUANDAA MKAKATI WA KUHAKIKISHA SOKO LA BIDHAA LINAKUWA NA BEI HALALI
Next articleDC SHIMO AAGIZA VIONGOZI KUSIMAMIA IMARA MIRADI YA MAENDELEO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here