Home LOCAL WATOTO WALIOWAHI KUKINZANA NA SHERIA MKOANI ARUSHA WAMSHUKURU RAIS SAMIA WAAHIDI KUWA...

WATOTO WALIOWAHI KUKINZANA NA SHERIA MKOANI ARUSHA WAMSHUKURU RAIS SAMIA WAAHIDI KUWA RAIA WEMA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na watoto waliowahi kukinzana na Sheria mkoani Arusha.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athuman Kihamia ofisini kwake alipofika mkoani humo kwa ziara ya kikazi.

Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Tullo Masanja akifafanua namna Idara ya Ustawi wa Jamii inavyowasaidia Watoto wanaokinzana na Sheria kupata marekebisho ya tabia katika mahabusu za watoto zilizopo nchini wakati wa kikao kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu na Watoto waliowahi kukinzana na Sheria mkoani Arusha.

Baadhi ya Watoto waliwahi kukinzana na Sheria mkoani Arusha wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipokuwa akizungumza nao.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Na: Mwandishi Wetu Arusha

Watoto waliowahi kukinzana na Sheria mkoani Arusha kwa nyakati tofauti  wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kwao wakiwa wakiwa mahabusu na hatimaye kupata haki zao.

Shukrani hizo zimetolewa na mmoja wa Mtoto aliyewahi kukinzana na Sheria Lotoi Laizer kupitia risala ya watoto waliowahi kukinzana na Sheria mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu aliyekutana na watoto hao Mkoani Arusha kwa lengo la kuwapa shime juu ya umuhimu wa mabadiliko ya mitazamo na mwenendo kwa ajili ya maisha yao sasa na baadaye.

Laizer amesema wakati wakiwa mahabusu ya Watoto walipata huduma muhimu za Chakula na afya wakati wote walipokuwa mahabusu mbali na kupata fursa ya kujifunza stadi mbalimbali za maisha.

“Tunamahukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu mpendwa kupitia kwenu wasaidizi wake alituwezesha kupata chakula na pale tulipougua, tulipatiwa matibabu stahiki na katu hatukujisikia wanyonge.” alisema Laizer.

Ameongeza kuwa maisha malezi katika mahabusu yamewawezesha

kubadilika kisawasawa na wako tayari kushirikiana na jamii katika kulijengea Taifa na wameiomba Jamii iwapokee na kuwaamini, kuwapenda na kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao.

Akizungumza katika Mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amesema  Serikali  inatambua umuhimu wa kuwatunza Watoto na kujali maslahi yao hivyo ni muhimu watoto kutimiza wajibu wao kwa kuwatii wazazi na kufuata maelekezo pamoja na kujiepusha makundi yanayoweza kuwaingiza katika vitendo vya kihalifu vinavyopelekea kukinzana na Sheria.

Aidha, amesema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha watoto wao wanakwenda Shule na kuhakikisha hawajihusishi na mambo mengine ikiwemo vitendo vya kihalifu vinavyopelekea kukinzana na Sheria.

“Nitoe rai kwenu Watoto kuwa watii na wenye kupenda Shule kwani itawasaidia katika maisha yenu, kuheshimu wazazi na walezi, kutii Sheria za nchi na kuwa mfano mwema kwa watoto wengine ili kuepuka kukinzana na Sheria” alisema Dkt. Jingu

Dkt. Jingu amewahakikishia Watoto hao kuwa Serikali itaendelea kuwashika mkono kwa kuwaunganisha na Taasisi mbalimbali  ili waweze kupata ujuzi na stadi mbalimbali zitakazowasaidia kujiendeleza na kuachana na makundi maovu.

Kwa upande wake Mmoja wa Mzazi wa Watoto hao Kunukula Eubariki ameishukuru Wizara chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali kwa kuhakikisha watoto waliokinzana na Sheria waliopo mahabusu na waliomaliza kesi zao wanapata stadi mbalimbali zitakazowasaidia kujiendeleza zaidi.

Serikali kupitia Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inasimamia jumla ya mahabusu tano nchini zilizopo katika Mikoa ya Arusha, Dar Es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya na Shule ya Maadilisho Irambo Mbeya yenye lengo la kuwahifadhi Watoto waliokinzana na Sheria wakati wakisubiri hatma ya mashauri yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here