Home LOCAL DC MTATIRO AMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI UJENZI WA MADARASA

DC MTATIRO AMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI UJENZI WA MADARASA

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro katikati,akikata utepe jana wakati wa hafla ya kupokea vyumba 122 vya Madarasa vilivyojengwa chini ya Mpango wa Maendeleo Kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19 katika wilaya hiyo ambavyo vimekamilika kwa asilimia 100,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Chiza Marando na wa pili kushoto Afisa Mipango Bosco Mwingira.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma Chiza Marando kushoto,akitoa taarifa ya kukamilika kwa ujenzi wa vyumba 122 vya madarasa kwa Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro kulia,wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa hayo yaliyojengwa chini ya Mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19 ambapo Halmashauri hiyo ilipokea zaidi ya Sh.bilioni 1.4 hata hivyo baada ya ujenzi huo kiasi cha Sh.milioni 127 zimebaki.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro akimpa zawadi Mkuu wa shule ya Sekondari Migomba wilayani humo Adinan Swai,baada ya kuwa wa kwanza kumaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyojengwa chini ya Mpando wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19 katika wilaya hiyo.

Na: Muhidin Amri,Tunduru

MKUU wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,amewapongeza wataalam wa Halmashauri ya wilaya Tunduru wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Chiza Marando, kwa kusimamia na kutekelezaji vizuri ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19 mwaka 2021.

Mtatiro ametoa pongezi hizo jana, wakati akipokea taarifa ya Utekelezaji wa ujenzi wa vyumba 122 vya madarasa katika shule za Sekondari na madarasa 9 ya shule za msingi shikizi zilizojengwa katika Halmashauri hiyo.

Alisema,ujenzi wa madarasa hayo ni katika juhudi za Rais Samia Hassan kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ambayo imeelekeza Serikali iliyopo madarakani, kutekeleza miradi ya kimkakati ya kitaifa ikiwemo vyumba vya madarasa kwa ajili ya kumaliza changamotoya ya madarasa katika shule shikizi na shule sekondari.

“Mkurugenzi kaka yangu Chiza Marando, nakupongeza sana kwani katika kipindi kifupi tangu ulipofika Tunduru,umefanya mambo mengi mazuri, nakuombea kwa Mwenyezimungu ukiondoka hapa Tunduru upande ukawe Ras au Katibu Mkuu wa wizara”alisema.

“ndugu zangu wananchi na walimu,sasa hivi tuna Mkurugenzi ambaye halali na wakati wote anayetembelea miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali,nataka kusema huu ndiyo utumishi wa umma na huyu ndiye Mkurugenzi tuliyemuhitaji katika wilaya yetu kwa muda mrefu”alisisitiza Mtatiro.

Alisema,katika utekelezaji wa miradi hiyo Mkurugenzi amebakisha zaidi ya Sh.milioni 127 kati ya Sh.bilioni 2.4 zilizopokelewa na Halmashauri ya Wilaya Tunduru kwa kujenga vyumba 122 vya madarasa,ambapo ameagiza fedha hizo zielekezwe kutatua changamoto katika sekta ya elimu.

Amewataka wanafunzi,walimu na wakuu wa shule kuhakikisha watunza madarasa hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Mtatiro alisema, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya mkakati wa Taifa,hivyo wanapaswa kutunza miundombinu ya elimu na mtu atakayeharibu au kuhujumu kwa namna yoyote ni lazima alipe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Chiza Marando alisema, walipokea jumla ya Sh.2,520,000,000 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19 ikiwemo ujenzi wa vyumba 122 vya madarasa kati ya hayo, 113 ya shule za sekondari na 9 ya shule za msingi shikizi.

Alitaja miradi mingine ni ujenzi wa nyumba za watumishi,Jengo la dharura katika Hospitali ya wilaya,Uhamasishaji chanjo dhidi ya Covid-19 na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.

Marando alisema,Sh.2,260,000,000.00 zimetumika kujenga madarasa 113 kwenye shule 23 za Sekondari,Sh.180,000,000.00 ujenzi wa madarasa 9 kwenye shule za Msingi shikizi 3 na Sh.80,000,000.00 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Bweni katika shule ya msingi Tunduru Mchanganyiko.

Alisema,ujenzi wa madarasa 122 sekondari 133 na elimu ya msingi 9 pamoja na utengenezaji wa seti 4,520 ya viti na meza kwa elimu ya sekondari na madawati 135 kwa elimu ya msingi umekamilika kwa asilimia 100.

Marando alisema, kazi zilizobaki ni usafi katika maeneo ya ujenzi na kazi zinazoendelea kwa sasa ni ujenzi wa jengo la dharula,nyumba ya Mganga mkuu na ujenzi wa Bweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.

Alitaja fedha zilizotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari ni Sh.2,377,532,179.42 na fedha zilizobaki ni Sh.62,467,820.58 na vifaa vya viwandani vyenye thamani ya Sh.64,685,993.21

Aidha alisema, wametumia Sh. 168,388,346.7 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa upande wa elimu ya msingi na wastani wa Sh.11,611,653.3 zimetumika kujenga ofisi nne za walimu na fedha zilizobaki ni Sh. 69,720,185.21 kati ya hizo Sh.5,034,192.00 ni thamani ya vifaa vilivyobaki.

Pia alisema, Mwezi Novemba 2021 Halmashauri imepokea Sh.300,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharula,Sh.90,000,000.00 kujenga nyumba ya Mganga Mkuu na Sh.6,514,747.00 ni za ufuatiliaji.

Akiongea kwa niaba ya Walimu,Mkuu wa shule ya Sekondari Mgomba Adinan Swai ameishukuru serikali kujenga madarasa hayo kwani yanakwenda kuongeza morali ya walimu kufundisha na wanafunzi kupenda kwenda shule.

Previous articleWATOTO WALIOWAHI KUKINZANA NA SHERIA MKOANI ARUSHA WAMSHUKURU RAIS SAMIA WAAHIDI KUWA RAIA WEMA
Next articleWAZIRI MKUU AMJULIA HALI MUFTI NA SHEIKH MKUU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here