Home LOCAL WAANDISHI WA HABARI WAFARIKI KATIKA AJALI MWANZA

WAANDISHI WA HABARI WAFARIKI KATIKA AJALI MWANZA


Taarifa za Mwenyekiti Mwanza Press Club

Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza  lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.

Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ng. Gabriel amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.

Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia.

Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.

Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo.

 Edwin Soko

 Mwenyekiti

 Mwanza Press Club

 11.01.2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here