Home LOCAL WAANDISHI WA HABARI WAFARIKI KATIKA AJALI MWANZA

WAANDISHI WA HABARI WAFARIKI KATIKA AJALI MWANZA


Taarifa za Mwenyekiti Mwanza Press Club

Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza  lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.

Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ng. Gabriel amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.

Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia.

Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.

Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo.

 Edwin Soko

 Mwenyekiti

 Mwanza Press Club

 11.01.2022

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.NNE JANUARI 11-2022
Next articleRAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA NGUO CHA BASRA TEXTILE ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here