Home SPORTS SIMBA KUSHUKA DIMBANI TENA DHIDI YA MLANDEGE

SIMBA KUSHUKA DIMBANI TENA DHIDI YA MLANDEGE


NA: Stella Kessy,

KIKOSI cha Simba leo majira ya saa 2:15 dhidi ya Mlandege katika michuano ya kuwani kumbe la Mapinduzi katika dimba la Aman.

Kikosi hicho kinashuka dimbani kikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Selem View Academy 2-0.

Akizungumza kocha mkuu wa kikosi cha Simba Pablo Franco,ameweka wazi kuwa atakuwa na programu maalum na majembe mapya ya kikosi hicho ili kuhakikisha wanaingia katika mfumo wake na kupata muunganiko wa pamoja wa timu ili kuwa na kikosi imara.

Amesema kuwa kikosi chake kinahitaji ushindi ili kujihakkishia  kupata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo.

Hata hivyo katika michuano hiyo imewajaribu wachezaji wake  wapya ambao ni  Sharraf Shiboub na Muivory Coast, Mounkoro Tenena, ambao kuna uwezekano wakasajiliwa katika kipindi cha dirisha hili dogo la usajili.

“Tupo kwenye kipindi cha usajili wa dirisha dogo, ni wazi kuwa matumaini ya kocha yoyote ni kuhakikisha anakuwa na kikosi bora, ndicho ambacho tunakifanya kwa sasa kwa kujaribu kuona ni nyota gani tunawasajili kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu” amesema

“Baada ya kukamilisha mchakato wa kusajili wachezaji bora, kazi kubwa itakayobaki kwangu kama kocha ni kuhakikisha natengeneza muunganiko, ambapo tayari nimeandaa programu maalum ili kupata matokeo bora kutoka kwa kila mchezaji.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here