Home LOCAL RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMEENDELEA KUWAJALI WANYONGE KWA KUONGEZA BILIONI 5.5 KWENYE...

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMEENDELEA KUWAJALI WANYONGE KWA KUONGEZA BILIONI 5.5 KWENYE MRADI WA TASAF-Mhe. Ndejembi

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anawajali wananchi wanyonge ndio maana ameongeza shilingi Bil. 5.5 kwenye Mpango wa TASAF ili kaya zote maskini ambazo ni walengwa wa mpango huo zinufaike.

Mhe. Ndejembi amesema licha ya Mhe. Rais kuelekeza fedha nyingi kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, ameona ni vema kutenga fedha zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini ambao kwa kiasi kikubwa unazisaidia kaya maskini kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini. 

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, imefanya kila kitu kuuongezea nguvu ya kiuchumi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili uweze kutekeleza vizuri Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini, hivyo ni jukumu la kila mlengwa kuitumia vizuri ruzuku anayoipata kuboresha maisha yake,” Mhe. Ndejembi amefafanua

 Ili kuboresha zaidi maisha ya walengwa hao, Mhe. Ndejembi amewataka walengwa kuona umuhimu wa kuunda vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitawawezesha kupata sifa kukopeshwa na Halmashauri

“Ninatamani kuona baada ya kuanzisha vikundi vyenu vya ujasiriamali muende Halmashauri kuomba mkopo wa asilimia kumi (10%) utakaowawezesha kufanya shughuli za maendeleo ambazo zitaboresha maisha ya familia zenu,” Mhe. Ndejembi amehimiza

Aidha, Mhe. Ndejembi amewaeleza wanufaika hao kuwa, kwa zile Kaya ambazo bado zinasubiri kuingia kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, utaratibu unafanyika na muda si mrefu wataingizwa katika Mpango huo.

Kwa upande wake mlengwa wa TASAF, Bi. Scolastica Tinga wa Kijiji cha Kipundi, amemshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Mlengwa huyo ameishukuru pia TASAF kwa kumpatia ruzuku iliyomuwezesha kujenga nyumba bora ya kuishi, kwani kabla ya kuanza kupokea ruzuku toka TASAF hakuwa na nyumba bora ya kuishi.”

Credit – Ofisi ya Rais Utumishi.

Previous articleRAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU CHAMWINO DODOMA
Next articleTAMASHA LA UTAMADUNI LA KILIMANJARO LITAFUNGUA UTALII WA KIUTAMADUNI DUNIANI – YAKUB
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here