Home LOCAL RAIS MWINYI AWASILI PEMBA KWA ZIARA YA KIKAZI

RAIS MWINYI AWASILI PEMBA KWA ZIARA YA KIKAZI


ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na viongozi wa Serikali alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba akiwa katika ziara ya kikazi ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar,kwa ajili ya kuzindua Miradi ya Maendeleo kisiwani Pemba kesho Januari 3,2022.(Picha na Ikulu).
Awali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dkt.Mwinyi aliagwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah ambapo baada ya kuwasili kisiwani humo akiwa amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi alipokewa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Matar Zahor Masoud. 

Akiwa kisiwani Pemba, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kesho Januari 3,2022 mapema asubuhi anatarajiwa kushiriki katika ufunguzi wa Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar huko Konde, Mkoa wa Kaskazini Pemba. 

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi baada ya shughuli hiyo anatarajiwa kuwasili Kinyasini Wete kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi Kiwanda cha kutengeneza Maji Safi Watercom (T) Ltd na baadae kuwahutubia wananchi.

Previous articleWAZIRI MKUU AVUTIWA KASI YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO
Next articleWACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WAASWA KUPUNGUZA MIGOGORO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here