Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MTANDAO WA WANAWAKE LAKI MOJA JIJINI DAR

NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MTANDAO WA WANAWAKE LAKI MOJA JIJINI DAR



NA: HAPPINESS SHAYO WMU.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amezindua Mtandao wa Wanawake Laki moja jijini Dar es Salaam unaohusika na kupambana na ukatili wa kijinsia pamoja na kukwamua wanawake kiuchumi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Masanja amewataka wanawake kushiriki kupinga ukatili wa kijinsia na pia kushirikiana katika kujenga uchumi wa Taifa. 

Kuhusu Sekta ya Utalii, Mhe. Masanja amewahamasisha wanawake kuwekeza katika Sekta hiyo ili kuinua vipato vyao akitolea mfano uwekezaji kwenye huduma za malazi, chakula, usafiri na nyingine nyingi.

Aidha, Mhe. Masanja ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza vyema Taifa na kuwaheshimisha watanzania na pia kuwa Mwanamke wa kuigwa kwa kuongoza njia kwa wanawake.

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO.

Previous articleSIMBA SC YAITIA ADAMU DAR CITY, YAIPIGA GOLI 6-0 BILA HURUMA
Next articleNGOJA NIWAAMBIE HUYU DC JOKATE ANAJUA JAMANI, HONGERA ZAKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here