Home BUSINESS BRELA YAHUDUMIA WATU ZAIDI YA 200, YATOA VYETI PAPO KWA HAPO JIJINI...

BRELA YAHUDUMIA WATU ZAIDI YA 200, YATOA VYETI PAPO KWA HAPO JIJINI DAR


Afisa Leseni wa BRERA Robert Mashika (kushoto) akimkabidhi Cheti Mohammed Mseja (kulia) mara baada ya kufanikisha kufanya usajili wa Biashara yake mpya na kupatiwa cheti chake papo kwa hapo Katika viwanja vya Mlimani City ambapo BRELA inaendesha zoezi la kukutana na wananchi mbalimbali kutatua changamoto zinazoikabili zikiwemo za Usajili wa Majina ya Biashara zao na Makampuni.

Afisa Leseni wa BRERA Robert Mashika (kushoto) akizungumza na wateja waliofika mezani kwake kwa lengo la kupata huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa Biashara zao.

Afisa Leseni wa BRERA Sada Kilabula (wa kwanza kushoto akiwa na Afisa Usajili wa Taasisi hiyo Ruth mmbaga (katikati) wakimsikiliza Mbunifu wa alama za Barabarani kwa walemavu Jutoram Kabatele alipofika kwaajili ya kukamilisha taarifa za Kampuni yake.

Afisa habari wa BRELA Sheila Mfunami (aliyesimama) akitoa Elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Mlimani City kwa lengo la kupata huduma mbalimbali Wakala zikiwemo za Usajili.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza viwanjani hapo wakisubiri kupatiwa huduma. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wameendelea kujitokeza katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa Lengo la kupata huduma  zitolewazo na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  (BRELA) ambapo zaidi ya watu 200 wamesikilizwa.

Katika zoezi hilo imeshuhudiwa wananchi mbalimbali wakifika viwanjani hapo na kuhudumiwa ambapo jumla ya Majina 25 ya Biashara, na Makampuni 15 yamesajiliwa.

Aidha katika zoezi hIlo kumefanyika Usajili wa Nembo ya Biashara sambamba na kutoa Vyeti vya Usajili papo kwa hapo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Afisa Leseni wa BRELA Robert Mashika amesema kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri kutokana na idadi kubwa ya watu waliofika leo kwa lengo la kusikilizwa na kusajili Biashara zao sambamba na  kupatiwa Vyeti vyao papo kwa hapo.

“Zoezi letu linaenda vizuri sana kuna idadi kubwa ya watu wanaofika kupata huduma, tukishawasikiza tunapata kufahamu changamoto zao na kuzifanyia kazi” Amesema  Mashika.

Na kuongeza kuwa.
“Changamoto za Usajili wa Majina ya Biashara na Makampuni tunazimaliza hapa hapa, tunamsaidia mteja kujaza taarifa zake na kumkadhi Cheti chake hapa hapa” Ameongeza.

Aidha amewataka wananchi wote hususani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kuchangamkia fursa hiyo ili kupata majibu ya maswali yao na  ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili zikiwemo mifumo ya mtandao.

Mmoja wa wananchi waliojitokeza viwanjani hapo na kufanikiwa kusajili Biashara yake mpya na kupatiwa cheti chake papo kwa hapo ni Mohammed Mseja, yeye  amefurahia kwa kufanikiwa kufanya usajili na kuondoka na cheti chake.

“Leo ndio mara ya kwanza nakutana na BRELA wamenihudumia vizuri sana lakini kilicho nifurahisha ni kupata cheti hapa hapa sikutegemea” Ameeleza Mohammed.

Pia amewashauri vijana wenzake wenye Makampuni bubu watumie fursa hiyo kukamilisha Usajili ili waweze kufanya shughuli zao kisheria.

Mwisho.
Previous articleNAIBU WAZIRI DKT. KIRUSWA ATOA AGIZO MUHIMU KWA MMILIKI WA MGODI LONGIDO
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO IJUMAA JANUARI 28-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here