Na: Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar . 28/12/2021.
Kiasi ya Wafanyabiashara 350 kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kushiriki Tamasha la biashara la Zanzibar linalotarajiwa kuanza Januari 02 hadi Januar 15 mwaka 2O22 katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini . .
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Malindi .
Amesema tamasha hilo litatoa fursa za kibiashara, kuongeza ujuzi na wigo kwa wajasiriamali wadogo wadogo wenye viwanda pamoja na Taasisi za Serikali zinazotoa huduma mbali mbali kwa jamii.
Alisema ni miaka minane tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo, kupitia Wizara ya Biashara ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Nchi zinazotarajiwa kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Uganda,Kenya, Misri, Burundi , Tanzania bara na wenyeji Zanzibar ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia na Ubunifu katika ukuaji wa Biashara .
lengo ni kukuza biashara kwa kutumia teknolojia ya kuuza na kununua bidhaa kwa njia ya mtandao na wajasiriamali wachanga kutumika na kuengezeka thamani .
Hata hivyo aliwataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la nane la biashara la Zanzibar kwa kununua bidhaa zenye ubora za ndani na nje ya nchi .