Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw.Ben Mwaipaja akizungumza mara baada ya kujaziwa mafuta kwenye gari lake ambalo alilikatia Bima kubwa kupitia NIC .Zoezi hilo limefanyika leo katika uzinduzi wa promosheni ya JIKAVE NA NIC uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Madereva Bodaboda Fire Kariakoo Bw.Jaffari Hassan akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya JIKAVE NA NIC ambapo katika hafla hiyo madereva bodaboda na magari ambao wamekata Bima kubwa kupitia NIC wamejaziwa mafuta.
Madereva bodaboda wakiwa kwenye foleni ya kujaziwa mafuta na Shirika la Bima la Taifa (NIC) katika uzinduzi wa promosheni ya JIKAVE NA NIC.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
NA: EMMANUEL MBATILO, Fufllshangwe Blog DAR
SHIRIKA la Bima la Taifa ((NIC) wamezindua promosheni ya JIKAVE NA NIC ambapo kupitia promosheni hiyo wateja 5,000 watakaokata Bima kubwa magari yao yatajaziwa mafuta kuanzia lita 5 hadi lita 100 kutegemeana na kiasi cha ada ya Bima watakacholipa.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye amesema promosheni hiyo itaisha mara tu magari 5,000 yatakapofikiwa hivyo basi amewataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo.
“Promosheni hii ni ya bchi nzima Bara na Visiwani na pale tu mteja atakapokata Bima kubwa atapokea ujumbe papo hapo utakaomjulisha namna ya kujipatia zawadi yake katika mkoa wake alipo”. Amesema
Amesema amewasihi watanzania kuchangamkia bidhaa za Bima nyingine ambazo NIC wanatoa kwa wateja wao ili waweze kufaidika na promosheni nyingi zinazoolewa na Shirika hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw.Ben Mwaipaja ameushukuru uongozi wa NIC kwa utaratibu ambao wameufanya hivyo ameridhika na huduma zinazotolewa na Shirika hilo na kuamua kukata Bima ya Gari yake kupitia NIC.
“Nawashauri wateja wengine wenye vyombo vyao vya moto, wananyumba zao wanataka kukatia Bima basi waje NIC ambayo imeboreshwa na inamabadiliko makubwa sana na ninashukuru kwa utaratibu huu na nimepata mafuta yangu asanteni sana”. Amesema Bw.Mwaipaja.
Nae Kiongozi wa Madereva Bodaboda Fire Kariakoo Bw.Jaffari Hassan ameishukuru NIC kwa promosheni hiyo kwani wao wamekata Bima mwezi uliopita na sasa promosheni hiyo imewangukiwa wao na kuweza kujaziwa mafuta kwenye pikipiki zao hivyo wataendelea kuwahimiza madereva wengine wa bodaboda waweze kukata Bima kupitia Shirika la Bima la Taifa NIC.
Credit – Fullshangwe Blog.