Home BUSINESS WETCU YATOA MAKISIO YA UZALISHAJI KILO MILIONI 15 ZA TUMBAKU 2021/2022

WETCU YATOA MAKISIO YA UZALISHAJI KILO MILIONI 15 ZA TUMBAKU 2021/2022

 

Na: Lucas Raphael,Tabora

CHAMA kikuu cha ushirika cha wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi mkoani Tabora (WETCU),kimesema kinatarajia wakulima wa zao hilo kuzalisha tumbaku kilo milioni 15 ambazo zitakuwa na thamani dola 24,750 milioni zenye thamani ya sh bilioni 56,925,000.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake meneja wa WETCU Samweli Jokeya alisema uzalishaji huo utatokana na vyama vya msingi (AMCOS) 107 ambavyo ni vyama hai kulingana na sheria za ushirika.

Jokeya alitoa wito kwa serikali kuangalia namna ya kuweka ruzuku ya mbolea na vifungashio kwani imepanda sana kiasi cha baadhi ya wakulima wachache kushindwa kumudu gharama hizo za mbolea.

Alisema imefikia mahali sasa baadhi ya wakulima wameshindwa kukisia namna ya kulima ekari ngapi kutokana kupanda kwa gharama za mbolea.

Akizungumzia changamoto kadhaa hasa hali ya hewa meneja huyo alisema hali ya hewa kwa sasa bado inatishia uzalishaji endapo mvua zitakuwa chache. 

Alitaja changamoto nyingine ni pembejeo kutofika kwa wakati na kodi ya zuio ya mapato ya mkulima ni mzigo kwao hasa asilimia 2% kiasi kwamba mkulima anakuwa kwenye wakati mgumu namna atavyokadiria alime vipi.

Jokeya alisema bado chngamoto nyingine ya baadhi ya wakulima ambao wamekuwa wakitorosha tumbaku kupeleka kuuza kwenye vyamba vingine hali ambayo imekuwa ikileta shida katika suala zima la vyama vya msingi.

Aidha alisema wapo pia wakulima wamekuwa waiuza pembejeo hali ambayo imekuwa ikiwaletea hasara bila wao kujua.

Hata aliongeza kuwa kama WETCU wamekuwa wakiendelea kutoa elimu juu ya namna ya mkulima wa zao la tumbaku atakavyonufaika endapo atazingatia kanuni za kilimo cha zao hilo.

Alisema WETCU imkuwa ikiendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya athari ya utoroshaji wa tumbaku na madhara yake kwa ujumla kwwani kosa kisheria.

Jokeya alisema endapo wakulima wa tumbaku watazingatia kanuni za kilimo cha tumbaku watanufaika zaidi na kuondokana na umasinikini sambamba na kulima pia na mazao mengine kama mahindi,aliseti na maharage.

Mwisho

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here