KIKOSI cha timu ya taifa ya soka la Ufukweni Tanzania leo wameibuka na ushindi 2-1 dhidi ya Comoros katika mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.
Huku katika mchezo wa kwanza Tanzania ilichezea kichapo kwa msumbiji kwa penati 3-4 katika dakika za mchezo walitoa sare ya bao 4-4.
Akizungumza baada ya mechi kumalizika Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni Boniface Pawasa amesema kuwa kupata ushindi katika mchezo huo umezidi kupata mweleko wa mechi nyingine.
“Mechi haikuwa nzuri sana kama vile tulivyopanga kwa sababu kubwa ya kupata matokeo haya ni uchovu sababu tumecheza mechi mbili ndani ya ya saa moja na nusu jambo ambalo lazima vijana wachoke” amesema
Ameongeza kuwa kikubwa wamefurahi kuingia katika hatua ya nusu fainali watakutana na wenyeji wa michuano hiyo Afrika kusini.
Amesema kuwa kikosi kinaendelea kujipanga vyema katika mchezo huo unaofuata.
Alitoa mwito kwa watanzania kuzidi kuiombea timu ya soka la ufukweni izidi kuipeperusha vyema bendera ya Taifa.