Home SPORTS TANZANIA YAFANYA VYEMA SOKA LA UFUKWENI YAICHAPA COMOROS 2-1

TANZANIA YAFANYA VYEMA SOKA LA UFUKWENI YAICHAPA COMOROS 2-1

 

Na: Stella Kessy

KIKOSI cha timu ya taifa ya soka la Ufukweni Tanzania  leo wameibuka na ushindi 2-1 dhidi ya Comoros  katika  mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.

Huku katika mchezo wa kwanza Tanzania ilichezea kichapo kwa msumbiji  kwa penati 3-4 katika dakika za mchezo walitoa sare ya bao 4-4.

Akizungumza  baada ya mechi kumalizika Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni Boniface Pawasa amesema kuwa  kupata ushindi   katika mchezo huo umezidi kupata mweleko wa mechi nyingine.

“Mechi haikuwa nzuri sana kama vile tulivyopanga  kwa sababu kubwa ya kupata matokeo haya ni uchovu sababu tumecheza mechi mbili ndani ya  ya saa moja na nusu jambo ambalo lazima vijana wachoke” amesemaAmeongeza kuwa kikubwa wamefurahi kuingia katika  hatua ya nusu fainali watakutana na wenyeji wa michuano hiyo Afrika kusini.

Amesema kuwa kikosi kinaendelea kujipanga  vyema katika mchezo huo  unaofuata.

Alitoa mwito kwa watanzania kuzidi kuiombea  timu ya soka la ufukweni izidi kuipeperusha vyema bendera ya Taifa.

Previous articleHABARI PICHA : WAJUMBE WA BODI MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI WA TUZ WAZURU TCRA
Next articleSIMBA SC ILIVYOTUA JIJINI MWANZA KUIVAA RUVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here