KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya kuivutia kasi Red Arrows katika mchezo wao wa kimataifa.
Mtanange huo utachezwa Novemba 29 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka ushindi ndani ya dakika 90.
Hata hivyo Simba imeangukia hatua ya Kombe la Shirikisho baada ya kuangukia pua katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwa ilinyooshwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na kuondolewa mazima.
Licha ya kwamba mchezo wa kwanza ugenini ilishinda mabao 2-0 imeondolewa kwa idadi ya kufungwa mabao mengi nyumbani.
Akizungumza kocha mkuu wa timu ya Simba Pablo Franco amesema kuwa mchezo dhidi ya Red Arrows utakuwa mgumu na wachezaji wanapaswa kujitoa asilimiab100 katika muda wote wa dakika 90 za machezo.
“Kwakweli Mechi itakuwa ngumu , tupo nyumbani inatupasa kujituma kwa asilimia 100 muda wote wa mchezo ili tupate ushindi, maandalizi yanaendelea vizuri na matarajio yetu ni kupata ushindi “amesema