Home SPORTS SERIKALI IMEJIPANGA KUSIMAMIA VYEMA TIMU ZA TAIFA: DKT. ABAS

SERIKALI IMEJIPANGA KUSIMAMIA VYEMA TIMU ZA TAIFA: DKT. ABAS

 


Mwandishi wetu.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas amesema kwamba Serikali imejipanga vyema  kuhakikisha timu za Taifa, Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia hatua ya makundi dhidi ya DRC Congo pamoja na timu ya taifa ya watu wenye ulemavu, Tembo Warriors katika michuano ya Afrika.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati anazungumza na waandishi wa habari   Dkt. Abbasi amesema kuwa katika kuelekea katika mechi ya Taifa Stars dhidi ya Timu ya Taifa ya DRC Congo, tukio lililofanyika ukumbi wa Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

Hata hivyo kikosi cha timu ya Taifa Stars kinatarajia  kushuka dimbani Alhamisi katika dimba la uwanja wa Benjamini Mkapa huku timu ya ya mpira wa miguu kwa watu wenye (Tembo Warriors) ambao watakuwa wenyeji ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 25, mwaka huu.

Pia kikosi cha  Stars kinaongoza kundi J, wakiwa na pointi 7 sawa na Benin ambayo inashika nafasi ya pili, DRC Congo wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 5 na Madagascar wakishika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 3.

Amesema kuwa  Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Taifa Stars inafanya vizuri katika michezo yote miwili, dhidi ya DRC Congo ambao tutacheza siku ya Alhamisi tarehe 11 Novemba, 2021 mechi ambayo ni muhimu kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya msimamo wa kundi letu.

Aliongeza kwa kuelekea kuwa,  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa atatembelea kambi ya Stars kwa ajili ya kutia hamasa na motisha kwa wachezaji wetu wanaoenda kupambania Taifa.

“Kuelekea mchezo huu wa Alhamisi Serikali haina tashititi wala jakamoyo, tumefanya maandalizi mazuri Kuelekea mchezo huo ikiwemo kupata nafasi ya mashabiki elfu 30 kuingia uwanjani kushuhudia na kusapoti timu yetu ya Taifa katika mchezo muhimu wa kuwania timu 10 ambazo zitawania kufuzu kucheza kombe la Dunia,”.

“Watanzania tunahamasisha kujitokeza kuisapoti timu yao, shabiki ni mchezaji wa 12 ambaye atakuja kuwatia moyo wachezaji wetu, kwani michuano hii ni tukio kubwa sana na fahari kwa kila mwananchi na nchi yetu  kwa hatua hii tuliyofikia,” alisema Dkt Abbasi.

Ameongeza kuwa  Serikali tayari imeshaandaa ndege kubwa kwa ajili ya wachezaji kwenda nchini Madagascar na kurudi baada ya mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya wenyeji hao.

Amewataka watanzania kuanzia leo kuanza hamasa ‘Vibe’ kila kona ikiwemo katika mitandao ya kijamii huku akiwataka bodaboda kuninginiza bendera za Tanzania kwa ishara ya hamasa kuelekea mchezo huo.

Dkt Abbasi amesema mbali na sapoti kwa Taifa Stars, Serikali imetoa kiasi cha shilingi Milioni 135 kusaidia mashindano makubwa ya Afrika ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu ambayo Tanzania ni wenyeji wa michuano hiyo inayotoa timu nane ambazo zitakwenda kucheza kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu.

“Tanzania tunawakilishwa na Tembo Warriors, huu ujio wa mashindano hayo ikiwa ni wenyeji ni ishara kubwa sana na dalili nzuri ya Taifa letu,” alisema Dkt Abbasi.

Kwa upande wa katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wilfred Kidao amesema kwa upande wa maandalizi ya Stars yanaendelea vizuri na kuishukuru Serikali kwa kutimiza vigezo vya Covid 19 na kuruhusiwa mashabiki elfu 30.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi na TFF tumeweka viingilio rahisi kwa VIP B na C ni elfu 5,000 huku mzunguko ikiwa ni elfu 3000, tumeweka bei rahisi ili kuwapa nafasi watanzania kuingia kwa wingi kusapoti timu yao,” alisema Kidao.

Naye mdau wa soka nchini, Azim Dewji ametoa jezo 2000 kwa wanafunzi ambao wataojitokeza kuisapoti Taifa Stars na kuwataka mashabiki wa soka kuungana na kuwa pamoja na kuweka pembeni ushabiki wa Simba na Yanga.

“Alhamisi tunatambua ni siku ya kazi basi tunaomba Serikali iweze kutoa nusu siku kwa watu kukaa maofisini na kuwepo kwa mapumziko na kuwapa nafasi watanzania kwenda uwanjani kutoa sapoti,”.

“Binafsi nimenunua tiketi 100 kwa wafanyakazi wangu na kuwapa nusu siku ya kufanya kazi baada ya hapo kila mmoja tunaongozana kuja uwanjani kuisapoti taifa Stars, hii iwe mfano kwa makampuni mengine”

Previous articleRC MAKALLA: MKANDARASI WA UJENZI WA KULINDA KINGO YA BAHARI ,LANDSCAPING NA GARDEN YA KISASA COCO BEACH AMEPATIKANA.
Next articleTANZANITE YAICHAPA DJIBOUTI 8-0
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here