Home BUSINESS RC MAKALLA: MKANDARASI WA UJENZI WA KULINDA KINGO YA BAHARI ,LANDSCAPING NA...

RC MAKALLA: MKANDARASI WA UJENZI WA KULINDA KINGO YA BAHARI ,LANDSCAPING NA GARDEN YA KISASA COCO BEACH AMEPATIKANA.

 


– Asema ni utekelezaji wa maelekezo Rais Samia suluhu Hassan kuwalinda wafanyabiashara kutokana Na mabadiliko ya tabia nchi.
 
– Asema Ujenzi unaanza rasmi wakati wowote kwa mawe kupangwa kuzuia kumomonyoka kwa kingo Za bahari, kuweka paving na palms kupendezesha.
– Asema Coco Beach itakuwa sehemu Bora ya mapumziko kwa wananchi. 
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amekabidhi kazi ya Ujenzi wa Kingo za Kuzuia maji ya Bahari kwenda kwenye Vibanda vya Wafanyabiashara eneo la Coco Beach ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyotoa juzi alipotembelea ufukwe huo.
 
RC Makalla amesema Mkandarasi huyo ataanza kazi ya kupanga mawe na kujenga Garden ya kisasa ya Vigae kwenye eneo la mbele ya Vibanda ambalo kwa Sasa limetawaliwa na vumbi.
 
Aidha RC Makalla amesema Serikali imedhamiria kufanya ufukwe wa Coco kuwa kimbilio la Wananchi kwaajili ya matembezi, mapumziko, chakula na vinywaji.

Previous articleRAIS MHE DK.HUSSEIN MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MSANII MAARUFU KUTOKA NCHINI INDIA IKULU ZANZIBAR.
Next articleSERIKALI IMEJIPANGA KUSIMAMIA VYEMA TIMU ZA TAIFA: DKT. ABAS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here