Home BUSINESS WAZIRI KITILA AWAALIKA WADAU WA SEKTA BINAFSI NA WAFANYABIASHARA KUSHIRIKI MAONESHO YA...

WAZIRI KITILA AWAALIKA WADAU WA SEKTA BINAFSI NA WAFANYABIASHARA KUSHIRIKI MAONESHO YA EXPO 2020 DUBAI

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi Latifa Mohamed Khamisi .
DODOMA.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo  amewaalika wadau wa  sekta binafsi na wafanyabiashara  kushiriki maonesho ya dunia ya Expo 2020 Dubai ambayo yameanza Oktoba mosi mwaka huu hadi Machi 31 mwakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma,Waziri Kitila amesema mwaka 2013 Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) ilichaguliwa kuwa wenyeji wa EXPO 2020 Dubai.

Amesema awali maonesho hayo yalipangwa kufanyika kuanzia Oktoba mosi 2020 hadi 31,Machi 2021 lakini changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19 yalisogezwa mbele na yameanza Oktoba 2021 na yanatarajiwa kumalizika mwakani Machi 31.

Waziri Kitila amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi 191 ambazo zinashiriki maonesho hayo ambapo uratibu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzbar kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade).

Amesema kutokana na changamoto ya UVIKO 19 waandaaji wa EXPO 2020 Dubai wanahamasisha wafanyabiashara duniani kote kutumia fursa ya soko mtandao ambao hauna tofauti na mitandao maarufu duniani.

“Napenda kutumia fursa hii adhimu kuwajulisha na kuwaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara  kushiriki maonesho ya dunia ya Expo 2020 Dubai kupitia programu mbalimbali  ambazo zimeandaliwa  ikiwemo ziara za kujifunza  na mikutano ya kibiashara(B2B).

Amesema programu hizo zinajikita katika teknolojia, mipango,miji na vijiji. elimu, ufundi na ubunifu, mifumo ya ufundishaji, fursa za utalii, michezo, mazingira na fukwe, usafirishaji na mawasiliano, kilimo uongezaji thamani wa mazao.

Amesema EXPO ni maonesho ya dunia yanayosimamiwa na Shirika la Kimataifa lijulikanalo kama Bureau of International Exhabition (BIE) lenye Nchi wanachama 195.

Waziri Kitila amesema waonesho hayo hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo hudumu kwa miezi sita yakiwa na kauli mbiu ya maonesho hayo ikiwa ni masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa Nchi washiriki.

Amesema Tanzania inatangaza miradi ya kimkakati kama kama vile mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP),reli ya kisasa (SGR) upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam ,ujenzi wa viwanja vya ndege  na kuimarisha usafiri wa anga “amesema.

Waziri Kitila amesema manufaa ya kushiriki maonesho hayo ni makubwa ikiwemo kuvutia na kushawishi upatikanaji wa mitaji katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kupata wabia wa uwekezaji watakaoendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi.

Vilevile amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa makampuni kujitangaza na kunadi bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini ili kupata masoko ya uhakika kimataifa.

“Maonesho haya yatatuwezesha kuvutia zaidi watalii kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini  na kujifunza utamaduni na desturi za kitanzania,”amesema


Previous articleDKT. ABBASI: SERIKALI YA RAIS SAMIA INA JAMBO NA MICHEZO
Next articleSTARS YAICHAPA BENIN 1-0
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here