Home SPORTS STARS YAICHAPA BENIN 1-0

STARS YAICHAPA BENIN 1-0

KIKOSI cha timu ya  taifa Tanzania leo  imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Katika dakika ya 6  Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema  lilidumu mpaka dakika ya 90.

Kikosi hicho cha  Stars inachonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ilicheza kwa utulivu mkubwa na kusaka ushindi wa haraka kipindi cha kwanza na baada ya kupata ushindi kazi ya ulinzi na kushambulia kwa kushtukiza iliendelea.

Beki wa Stars, Kennedy Juma ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakitumia nguvu nyingi jambo lililopelekea akaonyeshwa kadi ya njano.

Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.

Previous articleWAZIRI KITILA AWAALIKA WADAU WA SEKTA BINAFSI NA WAFANYABIASHARA KUSHIRIKI MAONESHO YA EXPO 2020 DUBAI
Next articleTANZANIA, RWANDA NA BURUNDI WARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MRADI WA RUSUMO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here