Home LOCAL TANZANIA, KENYA KUMALIZA VIKWAZO VYA KIUTAWALA DISEMBA

TANZANIA, KENYA KUMALIZA VIKWAZO VYA KIUTAWALA DISEMBA

Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimuleleza jambo Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Mwakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam


Mazungumzo baina ya wakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam

Na: Mwandishi Wetu, Dar

Tanzania na Kenya zimedhamiria kumalizia kuondoa vikwazo vya kiutawala vilivyosalia ifikapo Disemba 2021 baada ya kuondoa vikwazo 46 visivyokuwa vya kikodi.

Hayo yamesemwa wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula  na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu jijini Dar es Salaam ambapo takwimu zinaonesha urari wa biashara kati ya Nchi hizo umeongezeka mara sita zaidi baada ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Kutokana na hatua hiyo, Tanzania imeonekana kunufaika zaidi kwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kwa kuuza zaidi bidhaa zake nchini Kenya.

“Hii ni ishara nzuri kwa Tanzania lakini pia ni fursa kwa Tanzania na Kenya kuondoa umaskini kwa watoto wetu na ndugu zetu kupata ajira kwa wingi katika sekta ya biashara,” Amesema Mhe. Kazungu.

Pia Balozi Kazungu amemueleza Waziri Mulamula kuhusu azma ya Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa nchini na kisha kuhudhuria sherehe za Uhuru tarehe 9 Disemba 2021 ambapo alialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Kenya mapema mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania inaheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa awali wa kuondo vikwazo hivyo na dhamira ni kuwa ifikapo Disemba 2021 vikwazo vya kiutawala navyo viwe vimeondolewa ili kukuza zaidi mahusiano ya Kidiplomasia na Biashara baina ya Tanzania na Kenya.

“Tumekubaliana kuhakikisha ifikapo mwezi Disemba 2021 vikwazo vyote vya kitawala viwe vimetatuliwa azma yetu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa kwa Ustawi wa Diplomasia na biashara baina ya Tanzania na Kenya,” amesema Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Previous articleNAMUNGO YAAHIDI KUCHUKUA POINTI TATU MBELE YA AZAM.
Next articleKATIBU MKUU NISHATI ASEMA MICHEZO ITUMIE KUBORESHA AFYA NA UFANISI KAZINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here