Home SPORTS NAMUNGO YAAHIDI KUCHUKUA POINTI TATU MBELE YA AZAM.

NAMUNGO YAAHIDI KUCHUKUA POINTI TATU MBELE YA AZAM.

 Na:Stella kessy.

Kocha Msaidizi wa Namungo Godefroid Okoko amesema kuwa wanakitambua kikosi cha azam hivyo wamejipanga vyema kwa mchezo wa kesho kuhakikisha wanatoka na alama 3.

Katika mchezo huo utaopigwa katika dimba la Chamanzi nje kidogo na Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari kocha huyo amesema kuwa timu ya Azam ni timu kubwa tumepanga kufanya vyema na wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo huo.

Mpaka sasa Namungo ina jumla ya pointi 4 akiwa ameshinda dhidi ya Geita na kutoka sare na kagera.

Lakini pia wanakutana na Azam ambao wanajumla ya alama 1 wakiwa wametoka sare mechi yao dhidi ya Coastal na kifungwa na Polisi Tanzania.

Kwa upande wa Nahodha wa timu hiyo Khamis Mgunya anasema kuwa wamejitaarisha vyema katika mchezo huo.

“Mimi sina shaka na kikosi changu kikubwa kufuata maelekezo ya kocha ambayo ametufundisha ili kuweza kupata matokeo ya ushindi”

Ameongeza kuwa licha ya kuwa na jumla ya pointi 4 lkn kikosi kimejipanga kufanya vyema

Previous articleKIKOSI CHA AZAM BADO KIPO HIMARA: KOCHA MSAIDIZI BAHATI
Next articleTANZANIA, KENYA KUMALIZA VIKWAZO VYA KIUTAWALA DISEMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here