Home LOCAL TMA YATOA SEMINA KWA WANAHABARI JUU YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

TMA YATOA SEMINA KWA WANAHABARI JUU YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua warsha ya wanahabari iliyoandaliwa na TMA ili kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari juu ya kuripoti vizuri habari za hali ya hewa.

Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Rose Senyangwa (kulia mbele) akiwasilisha mada kwenye warsha ya wanahabari iliyoandaliwa kuwajengea uwezo juu ya kuripoti vizuri habari za hali ya hewa.

Wataalam kutoka TMA pamoja na wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.
 

Baadhi ya wanahabari wakiuliza maswali anuai kwenye warsha hiyo.

Baadhi ya wanahabari wakiuliza maswali anuai kwenye warsha hiyo. 
Baadhi ya wanahabari wakiuliza maswali anuai kwenye warsha hiyo



Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Joyce Makwata (kulia) akifafanua jambo kwa wanahabari kwenye semina hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa akifafanua jambo kwa wanahabari walioshiriki katika warsha hiyo ya kuwajengea uwezo, iliyofanyika mjini Kibaha.

Na: Mwandishi Wetu, Kibaha

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewapongeza wanahabari kwa kuendelea kuijuza jamii juu ya taarifa mbalimbali za mabadiliko ya hali ya hewa nchini zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Kauli hiyoimetolewa leo Mjini Kibaha na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a alipozungumza akifungua warsha ya wanahabari iliyoandaliwa na TMA ili kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari juu ya kuripoti vizuri habari za hali ya hewa.

Alisema TMA inatambua kazi nzuri inayofanywa na wanahabari kupitia vyombo vyao vya habari kwani imeongeza mwamko wa jamii kufuatilia taarifa hizo.

“Ni kipindi kirefu sasa tangu tumeanza kuwa na warsha kama hizi kwenu wanahabari mara kwa mara kila tunapokaribia kutoa utabiri wa msimu. Kwa hakika matokeo tumeyaona kwani kwa msaada wenu tumeona mwamko na uelewa wa jamii juu ya Taarifa za hali ya hewa kuongezeka,” alisema Dk. Chang’a.

Aidha alieleza kuwa TMA itaendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari ili kuhakikisha kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati.

Alisema lengo la warsha hiyo ni kuwaandaa wanahabari kupokea taarifa ya mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2021, ikiwa na kauli mbiu ya “Zingatia Tahadhari Kujenga Ustahimilivu”.

Alibainisha kuwa kuongezeka kwa mwamko na uelewa kuhusu taarifa za hali ya hewa kwa jamii zinapoifikia kwa uhakika ni muhimu kwani inasaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa zinapojitokeza.

“Hivyo, taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kupatikana kwa wakati pamoja na athari zake ili kuweza kujipanga na kujiandaa katika shughuli mbalimbali za uzalishaji.“ Alisema.

Credit – Fullshangwe Blog.   

Sehemu ya washiriki katika warsha ya wanahabari iliyoandaliwa na TMA ili kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari juu ya kuripoti vizuri na kwa usahihi habari za hali ya hewa. 
 
Sehemu ya washiriki katika warsha ya wanahabari iliyoandaliwa na TMA ili kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari juu ya kuripoti vizuri na kwa usahihi habari za hali ya hewa.
Warsha ya wanahabari iliyoandaliwa na TMA ili kuwajengea uwezo juu ya kuripoti vizuri na kwa usahihi habari za hali ya hewa ikiendelea.

 Credit – Fullshangwe Blog.

Previous articleRAIS SAMIA AKISALIMIANA NA WANANCHI WA TEGETA NA ZINGA BAGAMOYO
Next articleSHINDANO LA KUMSAKA MISS PWANI KULINDIMA SIKU YA KESHO WILAYANI KIBAHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here