Home Uncategorized SHINDANO LA KUMSAKA MISS PWANI KULINDIMA SIKU YA KESHO WILAYANI KIBAHA

SHINDANO LA KUMSAKA MISS PWANI KULINDIMA SIKU YA KESHO WILAYANI KIBAHA

Baadhi ya washiriki  wapatao 15 wa shindano la kuwania taji la miss Pwani kwa mwaka wa 2021 wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika maandalizi ya kinyng’anyoro hicho ambacho kinatarajiwa kufanyika siku ya kesho ijumaa Wilayani Kibaha.

Mmoja wa washiriki wa shindano la kumsaka mlimbwende wa miss Pwani 2021 Sara akiwa katika pozi baada ya kumaliza kufanya mazoezi.

NA VICTOR  MASANGU, PWANI.

KINYANG’ANYIRO cha shindano ambalo lilikuwa linasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa la kumsaka mlimbwende  atakayewania taji la miss Pwani linatarajiwa kufanyika siku ya kesho ijumaa katika ukumbi wa  Destiny hall uliopo eneo la kwa mathias  Wilayani Kibaha.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalumu ambao ulioandaliwa kwa ajili ya kuwatambulisha warembo hao mkurugenzi mtendaji wa Twiga Enternment Mariam Sheiban aka (Twiga)  ambaye  pia ndiye mwandaaji wa shindano hilo amebainisha kuwa maandalizi yote mpaka sasa yameshakamilika.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika shindano hilo jumla ya walimbwende wapatao 15 kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani watashiriki katika siku hiyo ambapo watapanda jukwaani katika kuonyesha mavazi ya ubunifu, vazi la ufukweni pamoja na vazi la usiku sambamba na kuonyesha vipaji walivyonavyo.

“Maandalizi ya shindano letu la kumsaka miss Pwani kwa mwaka huu wa 2021 yanakwenda vizuri na mipango yote tumeshaifanya na warembo wote wamekaa kambini wakijifua tangu agosti 28 mwaka huu wakiwa wanajifua katika eneo la Art Hotel  hivyo imani yangu siku hiyo mashabiki watapata burudani ya aina yake,”alisema Twiga.

Aidha aliongeza kuwa katika shindano hilo litaweza kupambwa na burudani mbalimbali za wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya pamoja na burudani nyingine kutoka kwa bendi ya muziki wa dansi kutoka kwa  Ruvu stars  ambao watashusha burudani ya aina yake ambayo haijawahi kutokea

Akifafanua kuhusiana na suala la kiingilio alibainisha tiketi za kawaida watakata kiingilio cha shilingi 10,000 /=(SILVER),  ambapo katika viti vya kawaida vitalipiwa kiasi cha shilingi elfu 35,000 /= (PLUTINUM),  huku viti maalumu (VIP) tiketi zake zitauzwa shilingi elfu 50,000/= (GOLD) na kwamba zimeshaanza kuuzwa katika baadhi ya vituo.

Kwa upande wa wadhamini Twiga Enternment,Mtanga Poly Machiner,Anne Stationar , Kiteshe Lodge&Pub,Marrgap-makeup,Gnail,Hair Reluxer, Destiny Hall, Meeting Point, Art Hotel, Kiduli Security,Black Eye Sucurity,  Recho Collection, pamoja na Smart Studio.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliwaomba mashabiki na wadau mbali mbali wa fani hiyo ya ulimbwende kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo na kwani pia kutakuwa na burudani nyingine ambazo zitafanyika za wasanii kutoka Mkoa wa Pwani.  

(CREDIT – FULLSHANGWE BLOG).

Previous articleTMA YATOA SEMINA KWA WANAHABARI JUU YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA
Next articleNFRA YANUNUA TANI 4,600 ZA MAHINDI YA WAKULIMA RUKWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here