Home BUSINESS TCB YAZINDUA JUKWAA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

TCB YAZINDUA JUKWAA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka (kushoto), akizungumza wakati wa Uzinduzi rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililoandakliwa na Benki ya Serikali ya Biashara TCB, hafla hiyo imefanyika makaop makuu ya nchi Jijini Dodoma wengine pichani ni , Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi, pamoja na Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Diana Myonga.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka akitembelea babanda ya wanawake wajasiliamali wakati wa Uzinduzi rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililoandakliwa na Benki ya Serikali ya Biashara TCB, hafla hiyo imefanyika makaop makuu ya nchi Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka (wapili kulia), akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya wajasiliamali walijitokeza wakati wa Uzinduzi rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililoandakliwa na Benki ya Serikali ya Biashara TCB, hafla hiyo imefanyika makaop makuu ya nchi Jijini Dodoma.

 Na: Mwandishi Wetu

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imejipanga kuwa taasisi kinara ya kuwahudumia wanawake nchini hili kuwakwamua kiuchumi kupitia suluhisho za kifedha ambazo zinazingatia changamoto zao kama wajasiriamali.

Katika kutimiza hazma hiyo, TCB jana ilizindua Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo lilijikita zaidi kujadili nafasi ya akina mama katika kukuza uchumi wa taifa. Na hili kuwa na matokea chanya, Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi, alisema midahalo kama hiyo itafanyika pia Zanzibar, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.

“Katika makongamano hayo, wanawake hasa wajasiriamali, watapata fursa ya kuifahamu vizuri TCB na huduma zake wezeshi huku wakibadirishana mawazo na uzoefu wa mambo mbalimbali,” Bw Moshingi aliwaambia washiriki.

Aidha, aliongeza kuwa jukwaa hilo litazingatia sana nafasi ya wanawake kuwa chachu ya uchumi na maendeleo na jinsi wanavyoweza kutumia fursa za kibiashara zinazopatikana TCB kupitia huduma na suluhisho zake mbalimbali.

Bw Moshingi alisema benki hiyo ina wajibika kuupa kipaumbele uwezeshaji wa wanawake baada ya serikali kuziunganisha shughuli zake na zile za iliyokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB).

“Uongozi wa Benki ya Biashara Tanzania unapenda kuishukuru Serikali kwa kuwa na imani na sisi na kuamua kutuunganisha na benki za TWB, Twiga Bancorp na TIB Corporate,” Bw Moshingi alisema katika wasilisho lake.

Hatua hiyo imeiimarisha TCB sokoni kiushindani na kuifanya iwe na msuli wa kifedha wa kuweza kulihudumia taifa kwa ufanisi.Hilo aliliweka bayana kupitia takwimu za kiutendaji zinazoonyesha mali na amana za TCB kuwa 1.04trn/- na 888bn/- mtawalia kufikia mwishoni mwa mwaka jana.

Wakati faida kabla ya kodi ya TCB iliongezeka kutoka 400m/- mwaka 2007 hadi 21bn/- mwaka 2020, ukopeshaji ndani ya kipindi hicho ulikua hadi 618bn/- kutoka 36bn/-.

Bw Moshingi pia alisema zipo huduma maalum zinazowalenga akina mama kama akaunti ya TABASAMU, dirisha maalum kwa ajili yao kwenye matawi yote ya benki na huduma za bima maisha kwa vikundi ambavyo wanachama wake wengi ni wanawake.

“Mikopo zaidi 120bn/- imetolewa kwa wanawake na tumekusanya amana za 11.9bn/- kupitia akaunti za vikundi zaidi ya laki tatu ambapo asilimia 85 ya wanachama wake ni wanawake,” mtendaji huyo alisema.

Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la ufunguzi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka, ambaye aliipongeza Benki ya TCB na viongozi wake kwa kuanzisha utaratibu huo wa kimaendeleo na kiuwezeshaji.

Alisema ubunifu huo wa hali ya juu ni nyenzo mahsusi ya kuwakomboa wanawake kifedha na kuwajengea uwezo kibiashara huku akiitaka benki hiyo kuwaonyesha fursa ilizonazo za kuwasaidia.

Kwa mujibu wa maofisa waandamizi wa TCB, lengo la jukwaa hilo si tu kuwawezesha wanawake wa Kitanzania kiuchumi bali pia kuwaimarisha kifedha na kuwajenga kibiashara ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

Walisema Jukwaa la Wanawake na Biashara la TCB linaendana na mpango wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika kusimamia na kumiliki uchumi wa taifa.

“Kwa muktadha huo benki na taasisi nyingine za fedha nchini zinawajibu wa kushiriki kutekeleza ajenda hiyo ya serikali na TCB imeonyesha mfano mzuri wa hilo,” walifafanua.

Jukwaa hilo jipya litaendeleza huduma jumuishi kwa ajili ya wanawake kupitia mikakati mbalimbali itakayowawezesha kufungua uwezo wao wa ujasiriamali na kuchangia mabadiliko kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa. 

Pia litajikita zaidi kwenye ufumbuzi wa changamoto zinazozikabili biashara zinazomilikiwa na kuongozwa na akina mama.

MWISHO.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here