– Asema azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kutatua Migogoro ya Wananchi.
– Ataka Mgogoro huo kufika Mwisho.
– Awapa pole Wananchi kwa Mgogoro wao kudumu muda mrefu.
– Awataka TFS kuacha matumizi Makubwa ya Nguvu.
– Sasa kukutana na Wizara tatu za TAMISEMI, Mliasili na utalii na Wizara ya Ardhi kupata ufumbuzi.
Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.
Kufuatia Mgogoro wa Ardhi wa muda mrefu baina ya Wananchi na Wakala wa Huduma za Misitu TFS juu ya Msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameahidi kushughulikia Mgogoro huo kwa kushirikiana na Wizara tatu zinazohusika.
RC Makalla ametoa ahadi hiyo wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza Migogoro ya Wananchi ambapo Leo ni zamu ya Jimbo la Ukonga ambapo amesema azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kushughulikia Mgogoro ya Wananchi.
Miongoni mwa kilio Cha wananchi hao ni Matukio ya kupigwa, kuteswa na kukamatwa kwa Wakazi wanaozungukwa na Msitu huo ambapo RC Makalla amewaelekeza TFS kuacha matumizi Makubwa ya Nguvu na badala yake busara itumike.
Aidha RC Makalla amesema wakati anaendelea kushughulikia Mgogoro huo ni vyema TFS ikashirikiana na Wananchi hao na kupiga marufuku vitendo vya kukamata Wananchi wa Dar es salaam na kupeleka Wilaya ya Kisarawe.