RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Michezo kwa Wanawake ( Tanzanite Festival), litakalofanyika Viwanja vya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 16 hadi Septemba 19 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas, amesema siku ya kwanza ya tamasha kutakuwa na kongamano la kujadil michezo na kwamba mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wabobezi wa suala la michezo.
“Hali halisi kuelekea kwenye tamasha letu iko vizuri, tunawakaribisha sana wanawake wote wa Dar es salaam na wamikoani pia mje mnufaike na mambo mazuri na mengi ya wanawake,’’amesema.
Hata hivyo ametaja baadhi ya mada hizo ni uhalisi wa wanawake katika kushiriki michezo, maadili na taaluma ya michezo kwa wanawake pamoja na mchango wa vyombo vya habari katika michezo.
AmesemaTarehe 17 tamasha litapambwa na michezo nane ya wanawake kutoka katika timu vinara za taifa zikiwemo ngumi za wazi na kulipwa, Wanariadha kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Mpira wa Netibali utakaoshindanisha timu ya JKT Mbweni na Uhamiaji, Mpira wa miguu kati ya timu ya Simba Queen na timu ya Taifa ya U 20, Mpira wa wavu kati ya timu ya Jeshi stars na Magereza, Mpira wa kikapu kati ya timu ya Don Bosco na JKT pamoja na timu ya watu wenye ulemavu kwa mpira wa kikapu.
Alisisitiza kuwa vilabu vya michezo hiyo vimethibitisha kushiriki na kwamba siku ya tatu ya mashindano hayo michezo itamaliziwa kwa washidi kupewa zawadi na kwamba mgeni rasmi atakuwa Rais Samia.
Ameongeza kuwa lengo ni kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ambaye katika hotuba zake ameonekana mafanikio ya timu za wanawake lakini hazitangazwi kama za wanaume pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo kwani michezo ni ajira na hujenga afya.
Aliongeza kuwa lengo ni kuwapa nafasi Wanawake wanamichezo wenye vipaji mbalimbali kuonyesha uwezo wao Katika kukiza michezo.
Aliongeza kuwa kuna baadhi ya wasanii zaidi ya 30 ambao wamepanga kushiriki Katika tamasha hilo ambalo litakuwa na michezo Mingi ikiwemo ya asili kama rede,kuvuta kamba na netboli pamoja na mingine Mingi ambayo Katika Karne ya sasa haipo.
Hata hivyo alitoa mwito kwa wadau na washiriki kujitokeza Kwa wingi Katika tamasha hilo la michezo la Tanzanite.