Home ENTERTAINMENTS MBUNGE KAMONGA ATOA NG’OMBE WA KITOWEO TAMASHA LA NGOMA YA MGANDA LUDEWA

MBUNGE KAMONGA ATOA NG’OMBE WA KITOWEO TAMASHA LA NGOMA YA MGANDA LUDEWA

Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga akizungumza alipokuwa akifungua Tamasha la mashindano ya ngoma ya asili ya Mganda wilayani Ludewa, Njombe.(PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lifua, akisisitiza amani na utulivu wakati wa mashindano ya ngoma ya Mganda yaliyofanyika kijijini hapo.(PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).

Mbunge Kamonga akiwa na baadhi ya viongozi wakiangalia mashindano hayo.(PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).

Mashindano ya vikundi mbalimbali vya ngoma ya Mganda yakiendelea kwenye uwanja wa Nkinila, Lifua.(PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).

Watoto wakijifunya kupiga ngoma kwa kutumia kandambili zao wakati wa mashindano hayo. (PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).

Anaripoti: Richard Mwaikenda, CCM Blog, Ludewa.

MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga ametoa ng’ombe kwa ajili kitoweo kwa wanaoshiriki Tamasha la mashindano ya ngoma ya asili ya Mganda jimboni humo.


Akizungumza wakati wa ufunguzi Kamonga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mashindano hayo ya siku 3 ameipongeza kamati ya maandalizi  kwa kufanikisha tamasha linaloshirikisha maboma 15 kutoka wilaya za Mbinga, Nyasa na Ludewa yenyewe.


Amesema kuwa mashindano hayo ya ngoma ya asili yaliyofanyika katika Kitongoji cha Nkinila, Kijiji cha Lifua Kata za ya Luilo ni muhimu sana kwani husaidia kujenga mahusiano, huleta  burudani lakini pia amani na upendo na kwamba imo hata kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. (PICHA NA: RICHARD MWAIKENDA).


“Kwa hiyo ndugu zangu Michezo , Sanaa na Utamaduni inasisitizwa sana kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Serikali yetu ina wizara mahususi  ambayo husimamia mambo ya utamaduni, nimesikiliza nyimbo nimeona wanaimba nyimbo ya kudumisha amani upendo na mshikamano, ambao ulianzishwa wasisi wetu tokea miaka mingi, lakini michezo licha ya kuleta burudani, vile vile inatuburudisha na kujenga mauhusiano mema baina ya jamii,”amesema Kamonga.  (PICHA ZOTE NA: RICHARD MWAIKENDA).

Vikundi (maboma) vilivzoshiriki katika mashindano hayo ni:Wilaya za Ludewa;Lihagule,Luilo,Mseto,Idusi,Kiyoho, Nindi, Nsungu na Mzalendo. Nyasa ni;Lituhi,Taifa,Upendo, Uweyo na Shujaa na kutoka Mbinga ni Ndongosi na Lizombo. (PICHA ZOTE NA: RICHARD MWAIKENDA).

Mdau ili nisikuondolee uhondo nakuomba uendelee kuona/kusikiliza kupotia clip hii za video Mwenzekiti wa Kijiji cha Lifua,Msafiri Haule, Diwani wa Kata za Luilo, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Kamonga na wananchi wakizungumzia tamasha hilo lakini na kuona pia tamasha hilo. Credit – Blog ya Taifa ya CCM


Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TATU SEPTEMBA 6-2021
Next articleMALENGO TAMASHA LA NMB NA WABUNGE LAMVUTIA MAKAMU WA RAIS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here