Na: Mwandishi wetu,Dodoma
KLABU ya Simba imeimarisha Benchi lake la ufundi kwa kumteua kocha Hitimana Thiery kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Thiery ni mmoja wa walimu wanaeheshimika nchini Rwanda Lakini pia amewahi kuwa kocha msaidizi wa Gomes wakati wa Royan ikitwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo msimu wa 2021.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba Babra Gonizalez anasema kuwa Gomes aliipa klabu ombi la kuongezewa msaidizi mwingine kwenye Benchi la ufundi mwenye sifa za hitiman zinazokithi kila kitu.
“Ni jambo la kawaida kwa timu kubwa kuwa na kocha msaidizi zaidi ya mmoja Kutokana na mahitaji ya timu hiyo tumeamua kuongeza nguvu katika timu kwa kuwa na Mtu kama Thiery”anasema.
Kwa upande wake,Gomes ameeleza kufurahishwa na ujio wa Hitimana akisema kuwa ni mwalimu wa daraja la juu.
“Wakati nikija Afrika kwa mara ya kwanza mara nilianzia Rwanda na Rayon na ndio ilikuwa timu ya kwanza nakumbuka ilikuwa kali sana enzi zile na Hitimana alikuwa anasaidia kupooza joto kidogo ni mzuri lakini pia ni kocha wa viwango”anasema.
Hitimana ni msomi wa stashahada ya uzamili katika masuala ya fedha aliyopata nchini ubelgiji na ana leseni ya ukocha daraja A inayotolewa na CAF.
Hitimana ambaye ni raia wa Rwanda aliwahi kuifundisha Namungo FC pamoja na Mtibwa Sugar.