Home LOCAL CCM YAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE MAJIMBO YA USHETU NA KONDE

CCM YAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE MAJIMBO YA USHETU NA KONDE

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo September 10,2021 jijini Dodoma.

Ripoti ya: Alex Sonna, Fullshangwe Blog, DODOMA.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa katika kikao chake kilichoketi leo September 10,2021 Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma kimewapitisha wagombea ubunge wa majimbo ya Ushetu mkoani Shinyanga na Jimbo la Konde, kisiwani Pemba.

Hayo yamesema leo jijini Dodoma na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Shaka amesema kuwa Kamati Kuu ya CCM imempitisha Emmanuel Charehani kugombea ubunge katika Jimbo la Ushetu, nafasi ambayo ilikuwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Elias Kwandikwa.

Shaka ameeeleza kuwa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Ushetu zitazinduliwa Septemba 25 mwaka huu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Christine Mndeme.

Aidha amesema kuwa kikao hicho kimepitisha Mbarouq Amour Habib, kugombea ubunge katika Jimbo la Konde, nafasi ambayo ilikuwa wazi baada ya mbunge mteule wa jimbo hilo, Sheha Mpemba Faki, kujiuzuru.

Pia ameeleza kuwa kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo, zitazinduliwa Septemba 24 na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Juma Sadala, maarufu kama Mabodi.

Hata hivyo Shaka amesema kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwa kauli moja wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoiongoza serikali kwa kuwatetea, kuwasemea na kuwapigania Watanzania.

Amesema Rais Samia amesimama imara kuwatetea Watanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo tozo za miamala ya simu ambazo fedha zilizokusanywa zinatumika kujenga vituo vya afya 220 na madarasa zaidi ya 500.

Vile Vile Kamati Kuu ya CCM imempongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuchochea na kuendeleza upatikanaji maendeleo kwa wananchi.

Amesema kuwa Ziara aliyoifanya, Rais Dk. Mwinyi, hivi karibuni kisiwani Pemba, imedhihirisha namna ambavyo Serikali ya Zanzibar inavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kiuchumi na kijamii”

Credit – Fullshangwe Blog.

Previous articleHITIMANA AONGEZWA BENCHI LA UFUNDI SIMBA
Next articleKIWANDA CHA MBASIRA FOOD NI FURSA MPYA YA SOKO LA MAZAO RUKWA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here