Home SPORTS HITIMANA AONGEZWA BENCHI LA UFUNDI SIMBA

HITIMANA AONGEZWA BENCHI LA UFUNDI SIMBA


Na: Mwandishi wetu,Dodoma

KLABU ya Simba imeimarisha Benchi lake la ufundi kwa kumteua  kocha  Hitimana Thiery kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Thiery  ni mmoja wa walimu wanaeheshimika nchini Rwanda Lakini pia amewahi kuwa kocha msaidizi wa Gomes wakati wa Royan ikitwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo msimu wa 2021.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba Babra Gonizalez anasema kuwa Gomes aliipa klabu ombi la kuongezewa msaidizi mwingine kwenye Benchi la ufundi  mwenye  sifa za hitiman zinazokithi kila kitu.

“Ni jambo la kawaida kwa timu kubwa kuwa na kocha msaidizi zaidi ya mmoja Kutokana na mahitaji ya timu hiyo tumeamua kuongeza nguvu katika timu kwa kuwa na Mtu kama Thiery”anasema.

Kwa upande wake,Gomes ameeleza kufurahishwa na ujio wa Hitimana akisema kuwa ni mwalimu wa daraja la juu.

“Wakati nikija Afrika kwa mara ya kwanza mara nilianzia Rwanda  na Rayon na ndio ilikuwa timu ya kwanza  nakumbuka ilikuwa kali sana enzi zile na Hitimana alikuwa  anasaidia kupooza  joto kidogo ni mzuri lakini pia ni kocha wa viwango”anasema.

Hitimana ni msomi wa stashahada  ya uzamili katika masuala  ya fedha aliyopata nchini  ubelgiji na ana leseni ya ukocha daraja A inayotolewa na CAF.

Hitimana ambaye ni raia wa Rwanda aliwahi kuifundisha Namungo FC pamoja na  Mtibwa Sugar.

Previous articleMASHABIKI YANGA RUKSA MECHI DHIDI YA RIVERS UTD
Next articleCCM YAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE MAJIMBO YA USHETU NA KONDE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here