Home SPORTS CAF YAZUIA MASHABIKI YANGA

CAF YAZUIA MASHABIKI YANGA

Mwandishi wetu.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limezuia watazamaji katika mechi ya kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na Rivers United ya Nigeria kesho.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, CAF imezuia watazamaji katika mechi zote za Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa zinazochezwa Tanzania.

Yanga SC watakuwa wenyeji wa Rivers United kesho Saa 11:00 jioni katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.



Previous articleOFISI YA WAKILI MKUU WA SETIKALI IMEFANIKIWA KUOKOA ZAIDI YA BILIONI 541 KWA MWAKA FEDHA 2020/2021.
Next articleDIWANI BEATRICE AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here