Na: Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam Henry James amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Makurumla.
Mbali ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye Kata hiyo ambayo Diwani wake ni Bakari Kimwanga, James amepata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi na nyingine akiahidi kuzishughulikia ili kuhakikisha Kata hiyo inaondokana na changamoto.
Akiwa kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika Mtaa wa Mianzini katika Kata ya Makurumla,James amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na viongozi wa kata wakiongozwa na Diwani katika kusimamia miradi ya maendeleo.
“Nimekagua miradi ya maendeleo hakika nimeridhishwa na kazi iliyofanyika, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuboresha huduma za jamii ikiwemo miuondombinu mbalimbali,”amesema James.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo katika kikao sekta kwenye kata hiyo.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya yetu ya Ubungo, kipekee nimshukuru Rais Samia pamoja nawe chini ya usimamizi wako, tumepata miradi ya barabara yenye dhamani ya Sh.Milioni 420 ambayo tunaamini itakwenda kubadili sura ya kata yetu.
“Lakini kwa upande wa elimu tayari kea Shule tu ya Mianzini tumepata ujenzi wa madarasa ikiwa na ukarabati wa Sh milioni 47.5 na Kituo cha Afya tumepata Sh Milioni 15 ambazo zimejenga jengo la kufulia kwenye hospitali yetu asante sana mama Samia Suluhu Hassan nawe DC wako kwa usimamizi wako,” amesema Kimwanga
Mwisho