Home FASHIONS MBUNIFU NEAH ATAMBA KUITEKA MISS TANGA KESHO KWA MAVAZI YAKE

MBUNIFU NEAH ATAMBA KUITEKA MISS TANGA KESHO KWA MAVAZI YAKE

Na: MWANDISHI WETU
 
MBUNIFU chipukizi wa mavazi nchin Neah Pipoo ‘Neah Collection,’ anatarajia kuwavalisha washiriki wote 20 katika fainali itakayo fanyika kesho Tanga beach Resort.
 
Neah ambaye  ameshiriki katika matamasha mbalimbali ya mitindo hapa nchin ikiwemo Ledy in Red 2021 na  Runway bay Zanzibari, ambapo alitunukiwa tuzo ya Mbunifu Chipukizi 2020.
 
Akizungumza na waandishi wa habari wakati warembo hao walivyo tembelea ofisini kwake amesema amechukua miezi miwili kuandaa mavazi hayo.
 
“Nimefurahi kupata nafasi hii ya kuvalisha warembo wa Miss Tanga nitavalisha vazi la ubunifu, bichi, usiku na vazi la shoo ya ufunguzi hii ni frusa kubwa kwangu nimehakikisha washiriki hawa watapendeza na kuwa na muonekano nadhifu ambao haupingani na mila na desturi zetu,” anasema Neah.
 
Aliongeza kuwa mbali ya washiriki hao atamvalisha pia mtangazaji mashuhuri Dida Shaibu ambaye atakuwa mshereheshaji katika fainali hizo pamoja na muandaaji wa shindano hilo muigizaji Chuchu Hans.

Previous articleSTAMICO NA GST WAINGIA MAKUBALIANO YA KUIMARISHA UTAFITI KATIKA UCHIMBAJI MADINI
Next articleWIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA VYA MILIONI 300

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here