Home LOCAL MADIWANI DAR WAGOMA KUPITISHA TAARIFA ZA TARURA

MADIWANI DAR WAGOMA KUPITISHA TAARIFA ZA TARURA

NA: HERI SHAABAN

MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamegoma kupitisha na kujadili  taarifa za Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam.

Madiwani wa Dar es Salaam waligoma kupokea taarifa za (TARURA) katika kikao cha kawaida cha  baraza kilichokuwa kikijadili na kupitisha maendeleo ambapo walipitisha taarifa za Kamati  ambapo ilipofika hoja ya TARURA madiwani wa Jiji waligoma kupokea taarifa ya Barabara za TARURA kufuatia kushindwa kushiriki Meneja wa Wilaya yupo safari Kikazi  ambapo  katika baraza hilo alituma Msadizi wake.

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wote walinyoosha vidole na kushindwa kupokea taarifa mpaka hapo katika baraza lingine atakaporudi Mhandisi wa Wilaya ya Ilala wa TARURA.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu amelidhia hoja ya TARURA iwe iweke kipolo mpaka hapo  kikao kingine .

Akizungumza katika  baraza hilo Meya wa Dar es Salaam Omary Kumbilamoto  aliwataka kila Mkuu wa Idara awe anashiriki kikao mwenyewe bila kutuma mwakilishi .

Meya Kumbilamoto aliwataka madiwani wa Halmashauri hiyo  kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo kuongeza vyanzo vya mapato .

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala SADA MANDANGWA amelalamikia kata ya kariakoo kukosekana kwa Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata miaka yote mpaka sasa ambapo Diwani Sada alipendekeza katika baraza hilo wachukue eneo moja wapo ili wajenge Ofisi ya Kata  ikiwemo jengo la DDC Kariakoo .

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Ilala Mwalimu Beatrice Edward   alitoa kero yake iliyopo Mtaa wa Kitonga Upanga kuhusiana na Gereji Bubu ambapo alimshauri Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuwatafutia maeneo maalumu.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here