Home LOCAL NAIBU MEYA KIMJI AMEONGOZA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR...

NAIBU MEYA KIMJI AMEONGOZA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR KUPATA CHANJO YA UVIKO-19

 

NA: HERI SHAABAN

NAIBU Meya wa Halmashauri ya Dar es Salaam Saady Kimji amewaongoza Madiwani wa Halmashauri hiyo katika zoezi la kuchanjwa chanjo ya COVID  19 Leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Arnatogluo katika baraza la madiwani.

Naibu  Meya Kimji aliwataka wananchi wa Dar es Salaam na Wilaya ya Ilala kujitokeza kuchanjwa kila mmoja wetu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya COVID kwani chanjo hiyo ni hiyari .

“Madiwani wetu wa Halmashauri ya Jiji na wananchi Leo wameshiriki zoezi la chanjo ambalo linanafanyika Ofisi za Arnatogluo  kila siku kwa hiyari kila MTU.

Naibu Meya Kimji aliwataka wananchi wa Wilaya ya Ilala na Dar es Salaam kwa ujumla  kujikinga kwa kuvaa barako a na maji tiririka na kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo yanatolewa na Serikali.

Kimji aliwataka wananchi  kujilinda kila Wakati na wasiwe wanakaa katika mikusanyiko bila barakoa.

Mwisho

Previous articleCAF YAVUTIWA NA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI KATIKA MICHEZO NCHINI.
Next articleMADIWANI DAR WAGOMA KUPITISHA TAARIFA ZA TARURA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here