Home LOCAL KISWAHILI CHATENGEWA RASMI BAJETI YAKE SADC,SUALA LA KATIBU MTENDAJI MPYA LAACHWA MIKONONI...

KISWAHILI CHATENGEWA RASMI BAJETI YAKE SADC,SUALA LA KATIBU MTENDAJI MPYA LAACHWA MIKONONI MWA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI

 

Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC limepitisha rasmi bajeti kwa ajili ya kuhakikisha Kiswahili kinatumika katika ngazi zote za vikao vya SADC ikiwa ni pamoja na kutafsiri Mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo kwa lugha ya Kiswahili.

Uamuzi wa Baraza hilo la Mawaziri wa SADC umefikiwa katika siku ya pili ya kikao cha Bazara la hilo kinachoendelea Lilongwe Nchini Malawi kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali na hivyo kuidhinisha bajeti itakayotumika kwa ajili ya Kiswahili ikiwa ni pamoja na kutafsiri nyaraka zote katika Kiswahili tofauti na awali ambapo Kiswahili kilitumika wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali pekee.

Baraza hilo la Mawaziri wa SADC wamepata fursa pia ya kupitia majina yanayopendekezwa kwa ajili ya kumpata Katibu Mtendaji mpya wa Jumuiya hiyo kutokana na Katibu Mtendaji aliyepo hivi sasa Dkt. Stergomena Tax kumaliza muda wake katika Jumuiya hiyo.

Hata hivyo jukumu hilo la kumpata Katibu Mtendaji mpya wa SADC limeachwa mikononi mwa Wakuu wa Nchi na Serikali ambao watakutana tarehe 17 na 18,Agosti,2021 Lililongwe Nchini Malawi ambapo watapitisha jina moja kati ya mawili yaliyowasilishwa kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Botswana. Mkutano huu wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaofanyika Lilongwe Nchini Malawi utakuwa ni Mkutano wa mwisho wa Katibu Mkuu Mtendaji aliyepo hivi sasa Dkt. Stergomena Tax anayemaliza muda wake wa miaka nane.

Pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekitumia kikao hicho cha Baraza la Mawaziri kuomba kuungwa mkono katika kinyang’anyiro cha kuchagua nchi ambayo itakuwa makao makuu ya Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency. (AMA) . Mpaka sasa Nchi za Namibia,Zimbabwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndizo zimeonesha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (AMA).

Previous articleCRDB BANK INTERNATION MARATHON 2021 YAFANIKIWA KUKUSANYA NUSU BILIONI KUSAIDIA AFYA NA MAZINGIRA
Next articleACT WAZALENDO WATUMA SALAMU KWA RAIS MTEULE ZAMBIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here