Home SPORTS DC KIGAMBONI MHE.FATMA NYANGASSA AZINDUA VIJANA JOGGING CLUB,KIGAMBONI

DC KIGAMBONI MHE.FATMA NYANGASSA AZINDUA VIJANA JOGGING CLUB,KIGAMBONI

 

Na: Mohamed Ngoma, Kigamboni – DAR ES SALAAM.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangassa amezindua rasmi klabu ya Jogging ya Vijana Wilayani Kigamboni ambapo ikiwa na lengo la kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi katika kuujenga mwili kuwa imara na kuufanya kuwa na Afya njema lakini ikiwa na lengo pia la kuhamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Katika hotuba yake Mhe Nyangassa amewataka Vijana kujitokeza kwa wingi katika kutumia fursa kubwa ya mikopo kutoka halmashauri isiyokuwa na riba katika kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Pia Mhe.Nyangassa ametoa shukrani kwa Uongozi wa Vijana chini ya Mwenyekiti wao Mathei Mponela na Katibu wao Yusuph Mabena pamoja na wageni waalikwa wote wakiwemo Uongozi wa Vijana Ngazi ya Mkoa (Dsm) Katibu Athony Kantala na K/Hamasa Eng.Ummy.

Aidha amewataka Vijana kuwa mstari wa mbele katika kuyasemea mazuri yote ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan katika jamii kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa ajili ya maslai mapana ya maendeleo ya Taifa letu la Tanzania haswa kwa kuwa msikivu na mfuatiliaji.

Viongozi mbalimbali wengine wa Chama, Jumuiya na Serikali wamehudhuria wakiwemo Mwenezi wa CCM (W) KG Ndg.Abdlah Pazzi,Mwenyekiti wa Wazazi (W) KG Ndg.Greyson Mwinkola,Mhe.Dalmia Tumaini (DAS) Wilaya ya Kigamboni,Afisa Maendeleo wa Vijana Wilaya ya Kigamboni Ndg.Veronica,Mhe.Omary Ngulangwa (Diwani kata ya Mjimwema),Mhe.Zacharia Mkundi (Diwani kata ya Vijibweni) na wengine wengi.
 

Previous articleENEO LA GERNERAL TYRE ARUSHA KUWA MTAA WA VIWANDA VYA SEKTA MBALIMBALI.
Next articleWAZIRI BITEKO: MADINI NI RASILIMALI YA TAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here