Home BUSINESS ENEO LA GERNERAL TYRE ARUSHA KUWA MTAA WA VIWANDA VYA SEKTA...

ENEO LA GERNERAL TYRE ARUSHA KUWA MTAA WA VIWANDA VYA SEKTA MBALIMBALI.

Waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo akiongea na waandishi wa habari katika kiwanda cha General Tyre mkoani Arusha.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo amesema serikali ipo katika mchakato wa kuiuisha kiwanda cha General tyre na kuwa mtaa wa viwanda vikubwa na vidogo kutokana na eneo hilo kutokidhi mahitaji ya kuendelea kufanya uzalishaji wa matairi.

Profesa Mkumbo aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichoacha kufanya uzalisha kwa muda wa zaidi ya miaka 10 kutokana na teknolojia ya uzalishaji kupitwa na wakati pamoja na matairi yaliyokuwa yamezalishwa kukusa soko ambapo amesema kuwa lengo la kufanya eneo hilo kuwa mtaa wa viwanda ni kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuleta ajira kwa watanzania hasa watu wa Arusha.

Alisema kuwa wamechagua maeneo machache yatayoweza kuanzisha mitaa ya viwanda ambayo yataweza kuleta tija nchi nzima ambapo wamechagua
eneo Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza na Arusha ambapo kwa Arusha wamechagua eneo la General tyre ambapo ndani yake kutakuwa na viwanda vikubwa na vidogo vidogo bingo.

Alifafanua kuwa watafanya upembuzi yakinifu kupitia shirika la taifa la maendeleo(NDC) ili waweze kupata ushauri wa kitaalamu ni aina gani ya viwanda vinaweza kukaa katika eneo hilo na kwa kuzikatia uzuri wa mji wa Arusha ili kuweza.

“Niwaambie wananchi wa Arusha kuwa ni kweli kiwanda hiki kiliacha kufanya uzalishaji tangu mwaka 2007 na kupoteza ajira zaidi ya 400 lakini katika muda mfupi ujao kupitia uongozi wa Muheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu tutaenda kutumia eneo hili vizuri kupata mtaa wa viwanda vya kueleweka ndani ya eneo hili na naamini litachochea maendeleo ya nchi,”Alisema. Profesa Kitila.

Alifafanua kuwa mitambo iliyopo katika kiwanda hicho haviwezi tena kufanya kazi ya kuzalisha matairi kutokana na kupitwa na wakati hali ambayo haitaweza kuzalisha matairi yatayoendana na uhitaji wa soko la hivi sasa.

Kwa upande Rhobi Satima kaimu mkurugenzi mwendeshaji wa shirika la taifa la maendeleo alisema kuwa uzalishaji wa tairi unahitaji eneo kubwa zaidi ya ekari 200 lakini eneo hilo lina ukubwa wa ekari 50 ambapo wameganya utafiti katika viwanda vingine vya nje ambavyo pia vinatumia eneo kubwa hivyo kufanya eneo kukosa mwekezaji kwaaji ya uzalishaji huo.

Leonard Mgoyo msimamizi wa kiwanda hicho kutoka NDC alieleza kuwa kiwanda hicho wafanyakazi waliachishwa kazi August 2019 lakini tangu mwaka miaka ya 1998 kiwanda hakijawahi kufanya uzalishaji angalau asilimia 50 ya uwezo wake japo uwezo upo ila tatizo ni mitambo kuwa ya kizamani na kinachozalishwa kutohitajika katika soko.

Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo alisema kuwa wanachangamoto kubwa ya ajira na wanaamini kufufuka kwa kiwanda hicho kutatoa mwanga wa serikali ya awamu ya sita ili wananchi wa Arusha waweze kupata ajira na serikali iweze kupata kodi zitakazotokana na uzalishaji utakaokuwepo
.

Previous articleNANDY ALAMBA DILI, BILINAS ANAPENDA WATOTO
Next articleDC KIGAMBONI MHE.FATMA NYANGASSA AZINDUA VIJANA JOGGING CLUB,KIGAMBONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here