NA: HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala Arch ,Ng’wilabuzu Ludigija amezitaka Bodi za Shule wasitumie uwanja wa siasa katika kuchaguana kusimamia bodi za shule zilizopo Wilaya ya Ilala .
Mkuu wa Wilaya Ludigija aliyasema hayo Dar es Salaam leo katika semina ya kazi ya Walimu Wakuu wa shule za sekondari za serikali na binafsi pamoja na Maafisa Elimu Kata kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salam na Idara ya Elimu Sekondari.
“Ninaagiza katika Wilaya yangu zikaguliwe Bodi za shule kila wakati ziwe hai pia wasichague wasimamizi wa bodi hizo wanasiasa katika sekta ya elimu “ alisema Ludigija
Ludigija aliwataka Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata kushirikiana na bodi za shule zao katika kukuza sekta ya elimu ndani ya Wilaya hiyo.
Aliwataka Wakuu wajue majukumu yao na masuala ya uwendeshaji kila Mkuu wa shule anasimamia ipasavyo ikiwa pamoja na ufundishaji,ujifunzaji kuakikisha mambo yanayowahusu walimu na Watumishi wasio Walimu na haki zao zinasimamiwa na kutekelezwa .
Aliwataka Walimu Wakuu wakae na kufanya tathimini kitaaluma katika mitihani ya ndani na mitihani ya Taifa katika kuweka mikakati yao sekta ya elimu kukuza taaluma Wilaya ya Ilala na kuongeza ufaulu.
Afisa Elimu Mkoa Dar es Salaam Alhaj Abdul Maulidi aliwataka Walimu wawe na nidhamu sambamba na usimamizi mzuri kwa watoto shuleni .
Alhaj Maulid alisema kazi yao ni wito hivyo wafanye kwa weledi na kudumisha nidham kazini ikiwemo kuboresha mazingira ya shule zao vizuri na kukuza taaluma na kuongeza ufaulu.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mussa Ally alisema dhumuni la kikao kazi hicho ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2022 Walimu Wakuu wa shule za Serikali pamoja na binafsi zilizopo Wilaya ya Ilala .
Mwisho.