Home Uncategorized MSHINDI MISS EAST AFRICA 2021 KUONDOKA NA NISSAN X TRAIL YENYE THAMANI...

MSHINDI MISS EAST AFRICA 2021 KUONDOKA NA NISSAN X TRAIL YENYE THAMANI YA SH.110,000,000.

Baadhi ya warembo wakishiriki uzinduzi rasmi wa zawadi ya gari jipya la kisasa aina ya Nissan x Trail,toleo la Mwaka 2021/21 lenye thamani ya shilingi 110,000,000 atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza atakaeibuka kidedea wa taji la Miss East Africa. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Makamu wa Rais wa Miss East Africa Beauty Pageant Joyli Mutesi (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano wao na wanahabari kutangaza rasmi kufanyika kwa shindano la Miss East Afica 2021 litakalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwezi Novemba 26 mwaka huu Jijini Dar es salaam. (wa kwanza kulia) ni Rais wa Taasisi hiyo Rena Callist na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko.
 

Makamu wa Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss East Africa Beauty Pageant Joyli Mutesi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) kwenye mkutano huo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss East Africa Beauty Pageant ),Rena Callist akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mashindano hayo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko akizungumzia ushiriki wa Serikali kwenye shindano hilo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Baadhi ya warembo wakishiriki uzinduzi rasmi wa zawadi ya gari jipya la kisasa aina ya Nissan x Trail,toleo la Mwaka 2021/21 lenye thamani ya shilingi 110,000,000 atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza atakaeibuka kidedea wa taji la Miss East Africa. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

DAR ES SALAAM.
Walimbwende kutoka katika nchi 16 za ukanda wa Afrika mashariki wanatarajia kuchuana vikali katika shindano la Miss East Africa yatakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mashindano hayo leo kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Rais wa mashindano ya urembo wa Afrika Mashariki (Miss East Africa Beauty Pageant ), Rena Callist amesema kuwa jumla ya zawadi za Sh.146,000,000 zitatolewa ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa gari Jipya la kisasa aina ya Nissan x trail toleo la mwaka 2021/21 lenye thamani ya sh. 110,000,000.

Aidha amesema kuwa Mshindi wa pili atapata pesa taslimu Sh. 11,000,000 na Mshindi wa tatu atajipatia Pesa taslimu 5,000,000 huku zawadi nyingine kwa washiriki wa mashindano hayo zenye thamani ya 20,000,000.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yatarushwa moja kwa moja na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii na kutarajiwa kuangaliwa na watazamaji zaidi ya milioni 300 Duniani kote ambapo Tanzania itapata fursa ya kutangaza vivutio vya utalii.

Nchi zilizothibisha kushiriki mashindano hayo ni pamoja na Tanzania, Kenya, uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan, Ethiopia, Elitrea, Djibouti, Somalia, Malawi, Visiwa vya Seychelles, Comoros, Madagascar, Reunion na Mauritius “Calist amesema”


Previous articleSERIKALI YAPUNGUZA TOZO YA MIAMALA YA SIMU KWA ASILIMIA 30
Next articleDC ILALA AZITAKA BODI ZA SHULE ISIWE UWANJA WA SIASA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here